Ansarullah ya Yemen: Marekani haina haki ya kuzihukumu nchi zingine
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i121846
Harakati ya Ansarullah ya Yemen iimetoa radiamali kwa hatua ya Marekani ya kuiweka Yemen katika orodha ya magaidi na kubainisha kwamba, Washington ambayo inahusika na mauaji ya Wapalestina na wasio na hatia haina haki ya kuzihukumu nchi zingine.
(last modified 2025-01-24T09:19:23+00:00 )
Jan 24, 2025 09:19 UTC
  • Ansarullah ya Yemen: Marekani haina haki ya kuzihukumu nchi zingine

Harakati ya Ansarullah ya Yemen iimetoa radiamali kwa hatua ya Marekani ya kuiweka Yemen katika orodha ya magaidi na kubainisha kwamba, Washington ambayo inahusika na mauaji ya Wapalestina na wasio na hatia haina haki ya kuzihukumu nchi zingine.

Ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen imetangaza katika taarifa yake kwamba Marekani ambayo mikono yake imetapakaa damu za watu wasio na hatia, haina sifa wala ustahiki wa kuzihukumu nchi na mataifa mengine na kuziweka katika orodha ya ugaidi.

Imekuja katika taarifa hiyo kwamba, kuingizwa harakati ya Ansarullah katika orodha ya ugaidi ni kitendo kkilichopitwa na wakati na hakina uhalali wowote isipokuwa kuutumikia Uzayuni.

Ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen imesisitiza kuwa: Uadui wa Marekani dhidi ya taifa la Yemen na utetezi wa kila upande wa Washington kwa  utawala wa Kizayuni kwa kutumia uwezo wake wote ni jambo ambalo liko wazi kwa mtu yeyote, na lengo pekee la hatua hiyo ya kidhalimu ya serikali mpya ya Marekani ni kuulinda utawala ghasibu wa Israel na kuunga mkono jinai zake dhidi ya taifa la Palestina.

Harakati ya Ansarullah ya Yemen imeongeza kuwa: Lengo la Marekani ni kuzidisha mateso kwa taifa la Yemen na kulizuwia taifa na majeshi ya nchi hiyo kuendelea kuliunga mkono taifa na kadhia ya Palestina.

Ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen pia imezitaka nchi na mataifa huru na taasisi za kisheria na za kibinadamu kulaani uamuzi huo usio wa kimaadili wa Marekani.