Oct 04, 2024 03:14 UTC
  • Ansarullah: Nasrullah alizima njama za Wazayuni katika eneo

Kiongozi wa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen sanjari na kutoa pongezi na mkono wa pole kufuatia kuuawa shahidi Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, amesema Sayyid Hassan Nasrullah alitibua njama za Israel na kuusababishia utawala huo dhalimu vipigo vya fedheha.

Abdul-Malik al-Houthi, Kiongozi wa Ansarullah ya Yemen alisema hayo jana jioni wakati wa akitoa hotuba kwa njia ya televisheni iliyorushwa moja kwa moja kutoka mji mkuu wa Yemen, Sana'a.

Amesema, “Adui wa Israel alimlenga Nasrullah kwa chuki kubwa na uhasama, kwa sababu ya nafasi yake kubwa katika kukabiliana na utawala huo. Alipenda sana kuanzishwa kwa uhusiano wa kirafiki na kidugu miongoni mwa Waislamu, na juhudi zake katika suala hili ni za kipekee na za kupigiwa mfano."

Al-Houthi ameeleza bayana kuwa, Sayyid Hassan Nasrullah alizuia njama za adui Mzayuni na kuwasababishia kushindwa kwa fedheha. "Kwa ajili hiyo, utawala wa Kizayuni unafuatilia malengo ya kinyama kutokana na mauaji yake. Unataka kupunguza ushawishi wa Hizbullah na mrengo wa Muqawama wa Lebanon katika kusimama dhidi ya utawala huo na kuunga mkono taifa la Palestina," ameongoza Kiongozi wa Ansarullah.

Marhum Sayyid Hassan Nasrullah

Amebainisha kuwa, Hizbullah imeibuka kuwa mrengo imara na wenye ufanisi mkubwa katika kukabiliana na adui Mzayuni tangu kuasisiwa kwake takriban miaka 40 iliyopita, na imepata ushindi aali na wa kuvutia katika hatua zake zote.

Kwingineko katika matamshi yake, Kiongozi wa Ansarullah amesifu na kupongeza shambulio la makombora la kulipiza kisasi la Iran, lililopewa jina la Operesheni ya Ahadi ya Kweli ya Pili, dhidi ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel. "Iran ilifanya shambulio kubwa zaidi la makombora dhidi ya Israel tangu kuanza kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina," ameongeza al-Houthi.

Tags