Ufaransa yashutumiwa kupanga kuangusha serikali pinzani barani Afrika
Ufaransa inapanga “mapinduzi ya kikoloni mamboleo” katika mataifa mbalimbali ya Afrika kwa lengo la kuangusha serikali inazoziona kuwa “zisizohitajika,” hususan katika eneo la Sahel ambako imepata pigo kubwa katika miaka ya hivi karibuni. Shirika la Ujasusi wa Kigeni la Urusi (SVR) limedai.
Hayo ni kwa mujibu wa tathmini ya Shirika la Ujasusi wa Kigeni la Russia (SVR), Paris imepoteza ushawishi wake katika baadhi ya makoloni yake ya zamani kufuatia wimbi la hisia kali za kupinga Ufaransa.
Burkina Faso, Mali na Niger zimevunja mahusiano na Ufaransa, zimefukuza wanajeshi wake na kuishutumu dola hiyo ya zamani ya kikoloni kwa kuunga mkono makundi yenye silaha yanayochochea uasi na ugaidi katika eneo la Sahel.
Ufaransa imesema haitatambua uhalali wa tawala za kijeshi katika nchi hizo tatu za Afrika Magharibi na imeapa kuunga mkono juhudi za kupindua serikali hizo.
Katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake ya habari Jumatatu, SVR ilisema serikali ya Ufaransa imekuwa “ikichunguza kwa pupa njia za kulipiza kisiasa” barani Afrika kufuatia mapinduzi ya kijeshi.
Kwa mujibu wa shirika hilo, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameidhinisha “vyombo vyake maalum” kuanzisha mpango wa kuwaondoa “viongozi wasiotakiwa” wa mataifa ya Afrika.
SVR pia imesema Ufaransa ilihusika katika jaribio la mapinduzi lililoshindikana nchini Burkina Faso tarehe 3 Januari, ikisema njama hiyo ilijumuisha mipango ya kumuua kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo, Ibrahim Traoré, ambaye ilimtaja kama “mmoja wa viongozi wa mapambano dhidi ya ukoloni mamboleo.”
Zaidi ya hayo, shirika hilo la kijasusi liliituhumu Paris kwa kujaribu kuyumbisha Mali kupitia mashambulizi dhidi ya misafara ya mafuta na juhudi za kuzingira miji, pamoja na kujaribu kuchochea machafuko katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. SVR pia imeunga mkono tuhuma za muda mrefu kutoka kwa mataifa ya Sahel kwamba Ufaransa “inatoa msaada wa moja kwa moja kwa magaidi” na inashirikiana na Ukraine kuwapatia wanamgambo ndege zisizo na rubani na wakufunzi.
Nchini Madagascar, ripoti ya kijasusi ilisema Ufaransa ilikuwa ikijaribu kumuondoa madarakani rais wa mpito, Michael Randrianirina, aliyeingia madarakani Oktoba 2025 kufuatia kuondolewa kwa rais wa zamani ambaye ni kibaraka wa Ufaransa, Andry Rajoelina.
Ripoti hiyo imekuja siku chache baada ya kiongozi wa mpito wa Niger, Jenerali Abdourahamane Tchiani, kuituhumu Ufaransa na nchi jirani kwa kufadhili mamluki waliohusika katika shambulio dhidi ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Niamey.
Ufaransa haijajibu madai haya ya hivi karibuni, ingawa hapo awali imekanusha tuhuma za kuunga mkono magaidi katika eneo la Sahel.