Washington Post: Iran ina uwezo wa kulenga kambi za kijeshi za Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i136170-washington_post_iran_ina_uwezo_wa_kulenga_kambi_za_kijeshi_za_marekani
Gazeti la Washington Pos limeripoti kuwa, Iran ina uwezo wa kulenga kambi za kijeshi za Marekani.
(last modified 2026-02-02T07:12:22+00:00 )
Feb 02, 2026 07:12 UTC
  • Washington Post: Iran ina uwezo wa kulenga kambi za kijeshi za Marekani
    Washington Post: Iran ina uwezo wa kulenga kambi za kijeshi za Marekani

Gazeti la Washington Pos limeripoti kuwa, Iran ina uwezo wa kulenga kambi za kijeshi za Marekani.

Likinukuu tathmini za usalama zilizofanywa na washirika wa Washington, gazeti la Washington Post limesisitiza kwamba Iran bado ina uwezo mzuri wa makombora na ina uwezo wa kulenga maslahi ya kijeshi ya Marekani, ikiwa ni pamoja na zaidi ya kambi 10 na makumi ya maelfu ya wanajeshi wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi.

Ripoti ya gazeti la Washington Post inasema, kulingana na tathmini iliyoandaliwa na mmoja wa washirika wa Marekani katika Ghuba ya Uajemi, Iran ina uwezo wa kudumisha silaha za masafa mafupi, majukwaa ya kurusha makombora, na uwezo wa kutengeneza makombora, na uwezo huu unaweza kuwa tishio kubwa kwa malengo ya Marekani katika eneo.

Kulingana na ripoti hiyo, uwezo wa Iran kutekeleza mashambulizi ya kulipiza kisasi kwa ufanisi umekuwa na jukumu muhimu katika hesabu za utawala wa Marekani wa Rais Donald Trump kwani uliongeza kupelekwa kwa vikosi vya Marekani kuizunguka Iran. Trump, ambaye hapo awali alikuwa amezungumzia uwezekano wa hatua za kijeshi, tangu wakati huo amebadilisha msimamo wake na kuitaka Tehran irudi kwenye mazungumzo ya nyuklia, hatua ambayo inapingana na kujiondoa Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA mwaka wa 2015.

Kwa mujibu wa uchambuzi uliofanywa na Washington Post, Iran imewaonyesha washirika wa Marekanikatika eneo kwamba ina uwezo wa kufanya mashambulizi mabaya katika Ghuba ya Uajemi, na iwapo kutatokea mzozo mpya, mashambulizi haya hayatazuiwa na kudhibitiwa.