Umoja wa Mataifa kutuma ujumbe wa kusimamia usitishaji mapigano nchini Congo DR
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i136218-umoja_wa_mataifa_kutuma_ujumbe_wa_kusimamia_usitishaji_mapigano_nchini_congo_dr
Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imetangaza kwamba ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Congo utatuma timu yake ya kwanza kusimamia usitishaji mapigano kati ya serikali na muungano wa "Mto Kongo", (Alliance Fleuve Congo) kwa Kifaransa, unaojumuisha harakati ya M-23, katika siku zijazo.
(last modified 2026-02-03T10:45:21+00:00 )
Feb 03, 2026 10:45 UTC
  • Askari wa UN nchini Congo DR
    Askari wa UN nchini Congo DR

Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imetangaza kwamba ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Congo utatuma timu yake ya kwanza kusimamia usitishaji mapigano kati ya serikali na muungano wa "Mto Kongo", (Alliance Fleuve Congo) kwa Kifaransa, unaojumuisha harakati ya M-23, katika siku zijazo.

Qatar ambayo ni mpatanishi katika mgogoro wa Congo DR imesema kwamba timu hiyo itapelekwa katika mji wa kimkakati wa Uvira mashariki mwa Congo.

Mji wa Uvira ameshuhudia mapigano baada ya waasi kuudhibiti mwezi Disemba, yakifuatiwa na kurejea vikosi vya jeshi la serikali na wanamgambo washirika katika mji huo, mwezi uliopita.

Tangazo la kutumwa timu ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa katika mji wa Uvira linaonekana kama ishara ya maendeleo katika mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Kinshasa na muungano wa waasi yanayosimamiwa na Qatar.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar pia imetangaza kwamba Jamhuri ya Kidemokraia ya Congo na waasi wamekubaliana kuhusu vipengee marejeo kwa ajili ya utaratibu wa kufuatilia usitisha mapigano ulioanzishwa chini ya makubaliano yaliyofikiwa Oktoba, na kuthibitisha tena uwajibikaji wao chini ya mfumo mpana wa makubaliano ya amani uliosainiwa Novemba mwaka jana.

Jitihada za sasa za kuimarisha mfumo wa kusimamia usitishaji mapigano zinakuja huku mapigano yakiendelea mashariki mwa Congo.

Serikali ya Congo imetangaza kwamba ndege zisizo na rubani zililenga uwanja wa ndege unaohudumia mji wa Kisangani kaskazini mashariki mwa nchi mwishoni mwa juma lililopita.