-
Harakati ya Ansarullah yawaachia huru mateka 350 wa vita vya Yemen
Sep 30, 2019 09:24Kamati ya mateka ya harakati ya Ansarullah ya Yemen imetangaza kuwa, harakati hiyo imewaachia huru mateka 350 wakiwemo mateka watatu raia wa Saudi Arabia ikiwa ni katika kutekeleza makubaliano ya amani ya Stockholm.
-
Nchi nane za dunia zaunga mkono tangazo la usitishaji vita la Answarullah ya Yemen
Sep 28, 2019 04:34Wajumbe wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani, Kuwait na Sweden, zimeunga mkono tangazo la usitishaji vita la Harakati ya Kiislamu ya Answarullah nchini Yemen.
-
Ansarullah: Mashambulizi yajayo dhidi ya Saudia yatakuwa makali zaidi
Sep 22, 2019 04:08Harakati ya Ansarullah ya Yemen imeapa kutoa majibu makali zaidi na yanayoumiza dhidi ya Saudi Arabia iwapo muungano vamizi unaoongozwa na utawala wa Aal-Saud hautasitisha uvamizi wake, mzingiro na mauaji dhidi ya wananchi wa Yemen.
-
Abdul-Salam: Damu ya wananchi wa Yemen ni 'nzito' kuliko mafuta ya Saudi Arabia
Sep 18, 2019 03:19Msemaji wa Harakati ya Wananchi wa Yemen ya Ansarullah ameitaka jamii ya kimataifa kulaani jinai za Saudia Arabia huko Yemen badala ya kuwalaumu Wayameni kwani damu za wananchi hao ni nzito na zenye thamani zaidi kuliko mafuta ya Saudia.
-
Answarullah: Ndege zisizo na rubani zinazoishambulia Saudia, zinatengenezwa Yemen
Sep 16, 2019 02:56Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa wa Harakati ya Wananchi ya Answarullah nchini Yemen, amesema kuwa ndege zisizo na rubani za jeshi la nchi hiyo, zinatengenezwa na Wayemen ndani ya ardhi ya nchi hiyo.
-
Moto wa Ansarullah waiteketeza ARAMCO; Saudia yatafuta njia ya kujigandua kwenye urimbo wa kinamasi cha Yemen
Sep 15, 2019 03:13Vituo vya mafuta vya shirika la mafuta la Aramco katika viwanda vya kusafisha mafuta vya Abqaiq na Khurais vilivyoko mashariki ya Saudi Arabia vimeteketezwa na moto mkubwa. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia imetangaza kuwa chanzo cha moto huo ni shambulio lililofanywa na ndege zisizo na rubani za droni.
-
Drone za Yemen zashambulia vituo vya mafuta vya shirika la Aramco la Saudia
Sep 14, 2019 07:01Ndege zisizo na rubani za harakati ya Ansarullah ya Yemen zimeshambulia kampuni mbili za shirika kubwa zaidi la mafuta la Saudi Arabia, Aramco.
-
Ubunifu wa Ansarullah wa kuunda jopokazi la mapatano jumuishi ya kitaifa
Aug 29, 2019 23:08Mahdi al-Mashat, Mkuu wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen ametangaza kuwa, limeundwa jopokazi linalojumuisha shakhsia 20 wa nchi hiyo kwa madhumuni ya kuleta mapatano jumuishi ya kitaifa na kutatua kisiasa mgogoro unaoendelea nchini humo.
-
Al Mashat: Umoja wa Mataifa una nafasi katika vikwazo vya chakula dhidi ya taifa la Yemen
Aug 22, 2019 01:04Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesema kuwa, Umoja wa Mataifa unachangia katika vikwazo vya kuingizwa chakula nchini Yemen kutokana na hatua yake ya kufungamanisha masuala ya kiuchumi ya nchi hiyo na kukaliwa kwa mabavu mji wa Aden.
-
Kiongozi wa Mapinduzi: Inalazimu kusimama na kukabiliana kwa nguvu zote na njama ya Saudia na Imarati ya kuigawanya Yemen
Aug 13, 2019 12:44Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, Saudi Arabia na Imarati zinataka kuigawanya Yemen; na akasisitiza kwamba: Inalazimu kusimama na kukabiliana kwa nguvu zote na njama hiyo na kuunga mkono Yemen moja, iliyoungana na yenye ardhi yake yote kamili.