Jan 28, 2024 06:38
Yemen, ambayo imekuwa ikizishambulia meli zenye uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel ili kuwahami na kuwaunga mkono Wapalestina wa Ukanda wa Gaza wanaoandamwa na mashambulio ya kinyama ya utawala huo, imesema inao uwezo wa "kuzizamisha" meli za adui mahali popote katika Bahari Nyekundu, ya Arabia na Mediterania.