-
Huduma mpya za Trump kwa utawala wa Kizayuni wa Israel
Jan 28, 2025 23:05Katika siku za mwanzo za muhula wake wa pili wa uongozi, Donald Trump, rais mpya wa Marekani, kwa mara nyingine tena amefuata njia ile ile aliyopitia katika muhula wa kwanza wa uongozi wake. Katika muhula wa kwanza, Trump alitoa uungaji mkono mkubwa na ambao haujashuhudiwa kwa utawala wa Kizayuni na kuchukua hatua mpya sambamba na kuiunga mkono Israel na kuwapinga Wapalestina. Vitendo na misimamo hii imekutana na majibu chanya kutoka Tel Aviv.
-
Kwa nini Trump hastahamili kuwepo kwa wahamiaji Waislamu huko Marekani?
Jan 27, 2025 23:23Moja ya amri tisa za Donald Trump katika siku ya kwanza ya uongozi wake ni kupitiwa upya sheria ya kurejesha marufuku ya Waislamu kuingia Marekani, suala ambalo iwapo litaidhinishwa na kutekelezwa, litakuwa na madhara makubwa kwa wahamiaji Waislamu nchini Marekani na hata waombaji visa Waislamu.
-
Rais wa Colombia alegeza kamba baada ya Trump kuamuru vikwazo dhidi ya nchi hiyo
Jan 27, 2025 03:44Rais Donald Trump wa Marekani jana alisema kuwa ataiwekea Colombia ushuru wa asilimia 25 na vikwazo baada ya nchi hiyo ya Amerika ya Kusini kukataa kuruhusu kutua nchini humo ndege mbili za kijeshi za Marekani zilizobeba wahamiaji waliofukuzwa huko Marekani.
-
Uroho wa Trump katika muhula wa pili wa urais wake
Jan 27, 2025 01:11Rais Donald Trump wa Marekani ameanza muhula wake wa pili wa uongozi huku akiweka hadharani uroho wake wa kupora ardhi, biashara na fedha za mataifa mengine ambapo ametangaza wazi azma yake ya kutaka kunyakua na kuunganisha ardhi za nchi huru na Marekani na pia kuhodhi kandarasi zenye faida kubwa kutoka kwa washirika wa Washington.
-
Mashirika ya haki za binadamu yatahadharisha kuhusu amri ya Trump ya kuwazuia Waislamu kuingia Marekani
Jan 26, 2025 03:37Wanaharakati wa haki za kiraia wameitaja amri mpya ya kiutendaji iliyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani inayowazuia raia wa nchi za Kiislamu kuingia Marekani kuwa ina taathira kubwa zaidi kuliko kile kilichoshuhudiwa mwaka 2017 na katika awamu ya kwanza ya serikali yake.
-
Ujio wa Trump; Marekani yawakamata na kuwafukuza mamia ya wahamiaji
Jan 24, 2025 23:26Katibu wa Habari wa Ikulu ya White House ya Marekani amefichua kuwa, katika wiki ya kwanza ya urais wa Donald Trump, wahamiaji haramu 538 wamekamatwa na kuzuiliwa, huku mamia ya wengine wakifukuzwa nchini.
-
Iran: Kuzishutumu nchi huru bila ya sababu ni kuendeleza uvunjaji wa sheria
Jan 24, 2025 00:07Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, tuhuma ya Marekani dhidi ya Cuba na kuliingiza tena jina la nchi hiyo katika orodha ya mataifa yanayodaiwa kuunga mkono ugaidi ni hatua ya kipuuzi na isiyokubalika kabisa.
-
Moscow: Marekani inachuma pesa kutokana na vita vya Ukraine
Jan 24, 2025 00:04Msemaji wa Kremlin amekosoa himaya ya kifedha na kisiasa ya Washington kwa serikali ya Kiev na kusema: Marekani inapata pesa kwa kuuza rasilimali zake za nishati za bei ya juu kwa watu wa Ulaya walioathiriwa na vita.
-
Madai ya Trump kuhusu maeneo ya nchi nyingine, dhihirisho la ubeberu wa hali ya juu
Jan 23, 2025 08:57Hatua isiyo ya kawaida ya Rais wa Marekani, Donald Trump, ya kutoa amri ya kubadili jina la "Ghuba ya Mexico" kuwa "Ghuba ya Marekani" imekabiliwa na hisia kali kutoka Mexico.
-
Maandamano ya Kwanza Dhidi ya Sera za Trump huko Washington
Jan 21, 2025 10:58Wakati ambapo Donald Trump, rais mteule wa Marekani, ameapishwa rasmi Jumatatu, tarehe 20 Januari, maandamano dhidi ya sera zake tayari yameanza. Katika muktadha huu, maelfu ya Wamarekani, wengi wao wakiwa wanawake, wamekusanyika katika mitaa ya Washington kuandamana dhidi ya sera za Trump.