-
WHO: Katika kila dakika 10 jeshi la Israel linaua mtoto mmoja Gaza
Nov 11, 2023 23:25Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, mtoto mmoja wa Kipalestina huuawa kwa wastani wa kila dakika 10 katika Ukanda wa Gaza na akatoa indhari kwa kusema "hakuna mahali popote na hakuna mtu yeyote aliye salama" chini ya mashambulizi ya Israel kwenye eneo hilo lililozingirwa.
-
Rais Raisi: Vita vya Gaza ni makabiliano kati ya mhimili wa sharafu na mhimili wa uovu
Nov 11, 2023 11:28Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika kikao cha pamoja cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kwamba: kadhia ya Gaza ni makabiliano baina ya mhimili wa sharafu na mhimili wa uovu, na kila mtu anapaswa abainishe yuko upande gani.
-
Kaburi la pamoja kuchimbwa ndani ya hospitali Gaza ili kuzika maiti 100 za waliouliwa na mashambulio ya Israel
Nov 11, 2023 09:24Wizara ya Afya ya Palestina katikia Ukanda wa Gaza imetangaza leo kuwa kaburi la pamoja litachimbwa ndani ya hospitali ya Al-Shifa ili kuzika maiti 100 zilizokuwa zimetawanyika hospitalini humo, za watu waliouawa shahidi kwa mashambulio ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Nchi za Kiarabu zinapaswa kukata uhusiano na utawala wa Kizayuni
Nov 10, 2023 08:07Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesisitiza ulazima wa serikali za nchi za Kiarabu kujibu ipasavyo matukio yanayojiri Ukanda wa Gaza na kusema: Jambo dogo kabisa linalotarajiwa kutoka kwa serikali za nchi za Kiarabu ni kukata uhusiano na utawala ghasibu wa Israel.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Mashinikizo ya kisiasa yazidishwe dhidi ya Marekani na utawala wa Kizayuni
Nov 06, 2023 10:49Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza udharura wa kuongezeka mashinikizo ya kisiasa ya Ulimwengu wa Kiislamu dhidi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel ili kusimamisha mauaji yanayofanywa dhidi ya watu wa Gaza na kusema: Iraq, ikiwa nchi muhimu katika eneo la Magharibi mwa Asia, inaweza kuwa na nafasi maalumu katika uwanja huu na kuanzisha mstari mpya katika ulimwengu wa Waarabu na wa Kiislamu.
-
Mpira wa kusimamisha au kupanua wigo wa vita Ghaza uko katika uwanja wa Netanyahu na jeshi la Kizayuni
Nov 05, 2023 03:22Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa inakaribia kufika mwezi mmoja tangu itekelezwe huku jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel likiendelea kuwaua watu wa Ghaza na kujaribu kufidia kushindwa kwao katika vita vya nchi kavu kwa kuwaua raia kwa umati.
-
Misimamo inayogongana ya White House na Biden kuhusu kusitishwa mapigano huko Ghaza
Nov 02, 2023 23:57Ikiwa zimepita takribani wiki 4 tangu kuanza operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa na mashambulizi ya jinai ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza ambayo yamepelekea kuuawa shahidi na kujeruhiwa maelfu ya Wapalestina hususan watoto na wanawake, Marekani ambayo ni muungaji mkono mkuu na mshirika wa kistratijia wa utawala wa Kizayuni, bado inataka kuendelezwa mauaji ya umwagaji damu huko Ghaza.
-
Kwa mara ya kwanza rais wa Marekani ataka kuwepo 'usitishaji' katika vita vya Israel dhidi ya Gaza
Nov 02, 2023 09:41Rais Joe Biden wa Marekani, kwa mara ya kwanza ametoa sauti ya kuunga mkono "usitishaji" mapigano kwa sababu za kibinadamu katika vita vya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza wakati Washington inatilia mkazo kuwaondoa Wamarekani wote waliokwama katika eneo hilo la Palestina lililowekewa mzingiro.
-
Kuendelea siasa za undumakuwili za Erdogan kuhusu uungaji mkono kwa watu wa Gaza
Nov 02, 2023 08:18Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki anaendeleza siasa zake za undumakuwili katika kuunga mkono watu wa Ghaza, huku ndege za kivita za kistratijia za Marekani zikiwa zimeegeshwa katika kituo cha kijeshi cha Incirlik kusini mwa Uturuki.
-
"Okoa watoto wa Gaza", Wamarekani wakatiza kikao cha Kongresi cha kumsaili Blinken na Austin
Nov 01, 2023 04:45Waandamanaji jana Jumanne walikatiza kikao cha kuwahoji mawaziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Marekani katika Bunge la Kongresi kilichoitishwa kwa ajiili ya kijadili suala la kuongeza uungaji mkono na misaada kwa Israel na Ukraine. Waandamanaji hao walioingia ndani ya Kongresi walitoa nara wakitaka "kuokolewa watoto wa Gaza" na "kusitishwa mapigano mara moja" katika eneo hilo la Palestina.