Mbunge wa Kizayuni: Kuuliwa watoto Gaza ni jinai
Mbunge wa utawala wa Kizayuni ameyataja mauaji ya watoto na wanawake wasio na hatia katika Ukanda wa Ghaza yanayofanywa na jeshi la utawala huo kuwa ni jinai.
Jumamosi, tarehe 7 Oktoba, wapiganaji wa Muqawama wa Palestina Hamas walitekeleza operesheni ya kushtukiza ya Kimbunga cha Al-Aqsa kutokea Ukanda wa Gaza dhidi ya maeneo ya utawala wa Kizayuni unaoikalia kwa mabavu Quds Tukufu, nao utawala huo ukaanzisha mauaji ya kinyama dhidi ya raia wa kawaida wa Palestina na kufunga vivuko vyote vya ukanda huo katika kulipiza kisasi na kufidia kushindwa kwake kijeshi na makundi ya mapambano ya ukombozi wa Palestina.

Kwa mujibu wa kanali ya Al-Jazeera Mubashar, Aidah Touma Suleiman, Mjumbe wa Knesset (Bunge la utawala wa Kizayuni), amekiri kuwa ni jinai kuua watoto na wanawake wa Gaza katika mashambulizi ya mara kwa mara yanayofanywa na jeshi la utawala huo huko Gaza.
Suleiman amesema: Ni lazima suala la kukamatwa watu wanaopinga vita katika utawala huu likomeshwe mara moja.
Mwakilishi huyo wa Kizayuni pia amekiri kwamba vita havisuluhishi lolote, bali huanzisha matatizo moja baada ya jingine.
Siku 43 baada ya kuanza operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, utawala ghasibu wa Israel umekuwa ukiendelea kulenga maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza, hususan majengo ya makazi na hospitali, na matokeo yake yamekuwa ni kuuawa shahidi zaidi ya Wapalestina 12,000, elfu 5 kati yao wakiwa ni watoto na elfu 3 300 wanawake.
Kulingana na Wizara ya Afya ya Gaza, zaidi ya Wapalestina 29,800 wamejeruhiwa, asilimia 70 kati yao wakiwa ni wanawake na watoto,