May 05, 2021 02:42
Mahmoud al Zahar, mjumbe mwandamizi wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds (Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani ambayo mwaka huu itasadifiana na Ijumaa ya keshokutwa ya tarehe 7 Mei) ni nembo ya mapambano ya haki dhidi ya batili na kusisitiza kuwa, shabaha ya kutangazwa siku hiyo ni kufanikisha ukombozi wa Palestina.