Pars Today
Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ameripotiwa amesema kuwa hatowachagua wanachama wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS kuwa mawaziri katika serikali yake endapo hawatokuwa tayari kutamka wazi na hadharani kuwa wanautambua utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imepinga vikali kuanza tena ushirikiano wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na utawala wa Kizayuni wa Israel katika masuala ya kiusalama.
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema utawala wa Kizayuni wa Israel ndio umehusika katika jaribio la mauaji lililofeli dhidi ya afisa wa ngazi ya juu wa harakati hiyo.
Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amezitaka nchi na pande zote za eneo la Mashariki ya Kati zikubaliane na fikra kwamba utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ndio "Hatari Kuu".
Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kuwa, harakati hiyo katu haitautambua utawala ghasibu wa Israel ambao umekuwa ukitenda jinai kila uchao dhidi ya wananchi wa Palestina.
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kuwa, jambo liloipambanua Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi nyingine ni uungaji mkono wake wa wazi kwa malengo matukufu ya Palestina.
Mkuu wa masuala ya kigeni wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, harakati hiyo ina hamu ya kustawisha uhusiano wake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nyuga zote.
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imesema hakuna mtu mwenye uwezo wa kuishurutisha harakati hiyo ya muqawama kuvunja tawi lake la kijeshi au kuutambua utawala haramu wa Israel kama masharti ya kukubali mapatano ya kitaifa ya Wapalestina.
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imesema kuwa inapinga mashatri yaliyotolewa na utawala wa Kizayuni ili kukubali mapatano ya kitaifa ya Wapalestina na kusisitiza kuwa mashatri hayo ni uingiliaji wa masuala ya Palestina.
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imetangaza kufikia mapatano ya maelewano ya kitaifa na chama cha Fat'h kwa lengo la kuhitimisha mgogoro wa kisiasa wa muongo mmoja kuhusu utawala wa Ukanda wa Ghaza.