-
Ijumaa, Julai 17, 2020
Jul 16, 2020 22:04Leo ni Ijumaa tarehe 25 Dhulqaada 1441 Hijria sawa na 17 Julai mwaka 2020.
-
Takwimu za leo za ugonjwa wa corona Iran, zaidi ya wagonjwa laki mbili na 30 elfu wapata afueni
Jul 16, 2020 08:00Msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran amesema, zaidi ya wagonjwa elfu mbili wa Covid-19 wamegunduliwa nchini katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita, huku idadi ya waliopata afueni ya ugonjwa huo ikipindukia 230,000.
-
Safari ya Abbas Araqchi mjini Kabul; ushirikiano mzuri wa Iran na Afghanistan
Jul 16, 2020 07:49Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu anayehusika na masuala ya kisiasa amekutana na kufanya mazungumzo mjini Kabul na Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Afganistan na kujadili masuala ya kupanua ushirikiano wa pande mbili katika nyanja zote
-
Russia na Ujerumani: Vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran havina maana
Jul 16, 2020 03:24Rais wa Russia na Kansela wa Ujerumani wamesisitiza kuwa, vikwazo vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran havina umuhimu wowote.
-
'Dawa ya kutibu virusi vya corona' iliyozalishwa hapa Iran kuingia sokoni karibuni
Jul 16, 2020 02:57Jamhuri ya Kiislamu ya Iran karibuni hivi itaanza kusambaza masokoni dawa ya kupambana na virusi ya 'Remdesivir' iliyozalishwa hapa nchini.
-
Abdollahian: Utawala wa Aal-Khalifa uimarishe uhusiano wa Wabahrain, si Israel
Jul 14, 2020 03:36Mshauri wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) katika masuala ya kimataifa ameukosoa vikali utawala wa Aal-Khalifa wa Bahrain kwa kukanyaga haki za binadamu za raia wa nchi hiyo.
-
Rais Rouhani: Iran itaibuka mshindi katika vita vya kiuchumi vya Marekani
Jul 13, 2020 22:49Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ushirikiano na mshikamano uliopo miongoni mwa mihimili mitatu ya dola, bila shaka utaipelekea Iran kuibuka mshindi katika vita vya kiuchumi vya Marekani dhidi ya taifa hili.
-
Hotuba ya Kiongozi Muadhamu katika mkutano na wabunge; sisitizo kuhusu majukumu na matarajio
Jul 13, 2020 03:06Ayatullah Sayyed Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu siku ya Jumapili alifanya mkutano kwa njia ya video na wabunge wa Awamu ya 11 ya Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la Iran ambapo amelitaja bunge hilo kuwa ni 'dhihirisho la matumaini na matarajio ya wananchi."
-
Iran yakanusha uvumi wa kuiuzia China kisiwa
Jul 12, 2020 23:10Iran imekanusha uvumi kuwa imeiuzia China kisiwa chake cha Kish katika Ghuba ya Uajemi na hali kadhalika imekanusha madai kuwa imeafiki kuiuzia China mafuta ghafi ya petroli kwa bei rahisi.
-
New York Times: Mapatano ya Iran na China ni pigo kubwa kwa Trump
Jul 12, 2020 08:40Gazeti la New York Times limechapisha sehemu ya waraka wa mapatano ya ushirikiano wa Iran na China na kusema kuwa mapatano hayo ni pigo kubwa kwa sera dhidi ya Iran za Rais Donald Trump wa Marekani.