-
Palestina yaikosoa UN kwa kutoiweka Israel katika orodha nyeusi ya wakiukaji wa haki za watoto
Jun 21, 2021 07:29Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Palestina imeukosoa Umoja wa Mataifa kwa kutoiweka Israeli kwenye orodha nyeusi ya kila mwaka ya makundi na nchi zinazohusika na ukiukaji mkubwa wa haki za watoto, ikisema kupuuza jinai za utawala huo kunawapa kinga ya kuhukumiwa Wazayuni wanaoua watoto.
-
Shakhsia 682 wa kisiasa wataka Biden akomeshe dhulma za Israel
Jun 19, 2021 21:53Mamia ya shakhsia wa kisiasa, wanaakademia, wanaharakati wa amani na washindi wa Tuzo ya Nobel wamemtaka Rais Joe Biden wa Marekani atimize ahadi yake ya kulinda haki za Wapalestina, na kukomesha dhulma za Israel.
-
Uhusiano wa Imarati na Israel wapigwa na dhoruba
Jun 16, 2021 07:53Siku chache baada ya kuanza utekelezaji wa makubaliano ya mafuta baina ya Abu Dhabi na Tel Aviv, Waziri wa Mazingira wa utawala haramu wa Israel ametoa mwito wa kufutwa mapatano hayo.
-
Wanahabari wa Afrika wataka Israel iwajibishwe kwa shambulio la Gaza
Jun 15, 2021 22:04Waandishi wa habari wa Afrika wameutaka Umoja wa Afrika (AU) ulaani mienendo ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuwashambulia wanahabari wa Palestina, sanjari na kuubebesha dhima kisheria utawala huo kwa jinai zake dhidi ya wanahabari.
-
Kuporomoka nduli wa Israel na kumalizika miaka 12 ya uwaziri mkuu wa Netanyahu
Jun 14, 2021 23:25Hatimaye nduli wa Israel, Benjamin Netanyahu ameporomoka kama walivyoporomoka makatili na nduli wote. Jumapili, Juni 13, 2021 bunge la utawala wa Kizayuni liliitisha kikao na kupasisha baraza jipya la mawaziri la Israel na kumbwaga Benjamin Netanyahu.
-
Majibu ya HAMAS kwa matamshi ya kichochezi na ya kujikomba kwa Wazayuni ya waziri wa Imarati
Jun 14, 2021 04:49Matamshi ya kichochezi yaliyotolewa na waziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) dhidi ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS, Hizbullah ya Lebanon na kundi la Ikhwanul Muslim, yamejibiwa na harakati ya HAMAS ya Palestina.
-
Netanyahu atupwa nje, Waisraeli washangilia, dunia yapongeza
Jun 14, 2021 03:38Benjamin Netanyahu ametimuliwa madarakani na kufikia tamati utawala wake wa miaka 12 katika utawala wa Kizayuni wa Israel. Hii ni baada ya bunge la utawala huo haramu (Knesset) kupiga kura ya kuidhinisha serikali mpya ya muungano jana Jumapili.
-
Wananchi wa Morocco wakataa majengo yao yageuzwe ubalozi wa Israel
Jun 13, 2021 21:59Wamiliki wa majengo na majumba katika mji mkuu wa Morocco, Rabat wamekataa kata kata kukodisha majengo yao kwa ajili ya kutumika kama ofisi za uwakilishi za utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Waandishi habari wa Marekani wataka kuakisiwa jinai za Israel katika vyombo vya habari vya nchi hiyo
Jun 12, 2021 22:20Zaidi ya Waandishi wa habari 500 wa Marekani wamesaini barua ya pamoja wakitaka kuakisiwa na kutangazwa habari zinazohusiana na dhulma na siasa za kibaguzi za Israel huko Palestina.
-
Nujabaa ya Iraq: Tuko tayari kuikomboa Miinuko ya Golan ya Syria
Jun 12, 2021 08:08Msemaji wa Harakati ya Muqawama ya Iraq ya al-Nujabaa ambayo ni sehemu ya harakati ya wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi ya nchi hiyo ametangaza utayarifu wa harakati yake kwa ajili ya kuikomboa Miinuko ya Golan ya Syria.