-
Zaidi ya Wapalestina 6,000 wametiwa nguvuni 2017; wanawake na watoto wanateswa kwenye jela za Israel
Dec 28, 2017 13:02Kituo maalumu cha Palestina kinachoshughulikia masuala ya mateka kimetangaza kuwa zaidi ya Wapalestina elfu sita wametiwa nguvuni na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika mwaka huu unaomalizika wa 2017.
-
Maandalizi ya Israel ya kuwafukuza Wapalestina wote katika mji wa Baitul Muqaddas
Dec 27, 2017 04:46Kutokana na baraka alizotoa Donald Trump kwa utawala wa Kizayuni kuhusiana na mji wa Baitul Muqaddas, bunge la utawala huo haramu limepanga kujadili rasimu ya sheria ya kuwafukuza Wapalestina wote katika mji huo kilipo kibla cha kwanza cha Waislamu.
-
Wapalestina 600 wamekamatwa tangu Quds itangazwe 'mji mkuu wa Israel'
Dec 27, 2017 03:50Mamia ya Wapalestina wamekamatwa na kuzuiliwa na maafisa usalama wa utawala haramu wa Israel tangu Rais Donald Trump wa Marekani aitangaze Quds Tukufu kuwa mji mkuu wa utawala huo wa Kizayuni mapema mwezi huu.
-
Israel inafanya njama za kudhibiti kikamilifu eneo la Ukingo wa Magharibi
Dec 26, 2017 11:51Chama cha Kizayuni cha Likud kimewataka viongozi na wawakilishi wa Bunge la utawala haramu la Israel kuhudhuria kikao cha dharura cha chama kwa ajili ya kuchunguza uamuzi wa kudhibitiwa kikamilifu na utawala huo, eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina.
-
Palestina: Uamuzi wa Guatemala kuuhamishia ubalozi wake Quds ni 'fedheha'
Dec 26, 2017 04:00Palestina imekosoa vikali hatua ya Guatemala ya kuuhamishia ubalozi wake Quds Tukufu kutoka Tel Aviv na kukitaja kitendo hicho kama 'fedheha'.
-
Askofu wa Waarmenia Tehran: Wakristo hawaitambui Israel
Dec 26, 2017 00:58Askofu wa Kanisa la Armenia mjini Tehran amesisitiza kuwa, Wakristo hawatambui serikali inayojiita Israel.
-
Wazayuni wavamia sehemu alipozaliwa Nabii Issa (Yesu) wawapiga mabomu Wakristo (+ Picha, Video)
Dec 24, 2017 13:11Bila ya kujali utukufu wa eneo alipozaliwa Nabii Isa AS, kwa mara nyingine jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limeuvamia mji wa Baytullahm (Bethlehem) na kuwashambulia kwa mabomu ya kutoa machozi Wapalestina waliokuwa wanaandamana kupinga siasa za kiuadui za Marekani dhidi ya eneo hilo takatifu.
-
Maandamano ya kuwapinga Wazayuni yaendelea nchini Tunisia
Dec 24, 2017 12:13Wananchi wa Tunisia kwa mara nyingine wameshiriki katika maandamano makubwa ya kupinga jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Hamas: Huenda Trump akaitambua Israel kama dola la Kiyahudi
Dec 24, 2017 04:34Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas, Ismail Haniya amesema amepokea taarifa za siri kuwa Washington inapanga kuutambua utawala haramu wa Israel kama dola la Kiyahudi.
-
Hamas yakaribisha takwa la ANC la kupunguzwa uhusiano wa kidiplomasia wa Afrika Kusini na Israel
Dec 22, 2017 12:13Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imekaribisha kwa mikono miwili takwa la chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kwa serikali ya nchi hiyo la kupunguzwa kiwango cha ushirikiano wa kidiplomasia wa nchi hiyo na utawala ghasibu wa Israel.