-
Afrika Kusini kuteremsha hadhi ya ubalozi wake huko Israel
Dec 21, 2017 12:48Afrika Kusini imesema kuwa itateremsha hadhi ya mahusiano yake ya kidiplomasia huko Israel ikiwa ni radiamali kwa uamuzi wa Marekani wa kuutambua mji wa Quds kuwa ni mji mkuu wa Israel.
-
UN yalaani kitendo cha Israel kumpiga risasi na kumuua Mpalestina mlemavu
Dec 20, 2017 04:50Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa amesema amestaajabishwa sana na kitendo cha jeshi la Israel kumuua kwa kumpiga risasi mtu mwenye ulemavu aliyekuwa anaelekea msikitini siku ya Ijumaa.
-
Iran yaalani hatua ya Marekani ya kulipigia kura ya veto azimio kuhusu Quds
Dec 19, 2017 04:09Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana usiku alilaani hatua ya Marekani ya kuupigia kura ya veto mswada uliopendekezwa na Misri kuhusu Quds na kuitaja hatua hiyo kuwa ni kinyume na amani na usalama wa kimataifa kwa lengo la kukandamiza haki za wananchi wa Palestina.
-
Marekani yatumia VETO kupinga azimio la Quds
Dec 19, 2017 00:56Licha ya wanachama 14 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuupigia kura ya ndio muswada uliopendekezwa na Misri kuhusu mji mtakatifu wa Baytul Muqaddas, lakini Marekani imeukwamisha muswada huo kwa kura yake ya veto.
-
Aoun: Israel inapanga kujenga ukuta wa kibaguzi kandokando mwa eneo la mstari wa bluu
Dec 18, 2017 23:19Rais wa Lebanon amesema kuwa utawala wa Kizayuni unatekeleza mipango ya kujenga ukuta wa kibaguzi kandokando mwa eneo linalojulikana kama "eneo la mstari wa bluu" huko Hasbaya karibu na mpaka wa Lebanon.
-
Mtego wa Israel kwa Saudia, kuwatenga Aal Saud na ulimwengu wa Kiislamu
Dec 15, 2017 02:39Gazeti la Kizayuni la Haaretz limetangaza kuwa, Yisrael Katz, waziri wa masuala ya kijasusi wa utawala wa Kizayuni wa Israel amemwita mjini Tel Aviv, Muhammad bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia.
-
Hamas: Hakuna nchi inayoitwa 'Israel' hata mji mkuu wake uwe 'Quds'
Dec 14, 2017 12:31Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imelaani vikali uamuzi wa Rais wa Marekani, Donald Trump wa kuitangaza Baytul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel na kusisitiza kuwa, hakuna dola linaloitwa Israel hata mji mkuu wake uwe Quds tukufu.
-
Wananchi wa Mauritania waandamana kumlaani Donald Trump
Dec 11, 2017 11:02Wananchi wa Mauritania wameungana na Waislamu na wapenda haki katika kona zote za dunia kuendeleza maandamano ya kumlaani rais wa Marekani, Donald Trump kwa hatua yake ya kuitambua Quds kuwa mji mkuu wa utawala pandikizi wa Israel.
-
Silaha za Marekani na Israel zapatikana katika ngome za ISIS, Syria
Dec 10, 2017 03:48Siku chache baada ya Mkuu wa Jeshi la Russia kutangaza kuwa genge la kigaidi la Daesh (ISIS) limeangamizwa kikamilifu nchini Syria, shehena ya silaha zilizotengenezewa Marekani na Israel imepatikana na wanajeshi wa Syria katika mji wa Dayr al-Zawr, iliyokuwa ngome ya mwisho ya magaidi hao.
-
Somalia yasema hatua ya Trump dhidi ya Quds ni 'hatari'
Dec 10, 2017 00:10Somalia imejiunga na nchi nyingine za Afrika kulaani hatua ya Rais wa Marekani, Donald Trump ya kuitangaza Baytul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.