-
Balozi wa Iran UN: Hatua ya Marekani kuhusu Quds ni kuhalalisha uvamizi na ukaliaji wa mabavu
Dec 09, 2017 04:03Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema, kukaliwa kwa mabavu Palestina ndilo chimbuko la migogoro yote ya eneo la Mashariki ya Kati na kusisitiza kwamba hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kuitangaza Quds kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni ni kujaribu kuhalalisha ukaliaji wa mabavu.
-
Wairani waandamana kulaani uamuzi wa Rais Trump kuhusu Baitul Muqaddas
Dec 08, 2017 11:29Maelfu ya wananchi wa Iran wameandamana leo baada ya Swala ya Ijumaa katika miji mbalimbali hapa nchini wakilalamikia na kulaani uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kuutambua mji wa Baitul Muqaddas wa Palestina kama mji mkuu wa utawala vamizi wa Israel.
-
Tanzania yapinga hatua ya Marekani kutambua Quds kama mji mkuu wa Israel
Dec 08, 2017 04:24Tanzania imetangaza rasmi kupinga uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani kutambua mji wa Quds (Jerusalem) kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Radiamali ya Umoja wa Ulaya kuhusu hatua ya Trump dhidi ya Quds Tukufu
Dec 08, 2017 01:18Federica Mogherini, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amelaani hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kutambua rasmi mji wa Beitul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Israel na kuongeza kuwa hatua hiyo ya upande mmoja bila shaka itavuruga utulivu wa ulimwengu na juhudi zote zilizofanywa kwa ajili ya kutatua mzozo wa Palestina.
-
Israel yaiuzia Sudan Kusini ndege zisizo na rubani
Dec 05, 2017 04:34Utawala wa Kizayuni wa Israel umeiuzia Sudan Kusini ndege zisizo na rubani na kamera za kisasa za usalama zilizogharimu mamilioni ya dola, licha ya nchi hiyo changa zaidi barani Afrika kusumbuliwa na ukosefu wa usalama, machafuko, njaa na wimbi la wakimbizi.
-
PLO: Kuuhamishia Quds ubalozi wa Marekani ni 'busu la mauti'
Dec 05, 2017 04:31Mwakilishi wa Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) nchini Marekani ameonya kuhusu madhara ya mpango wa Washington wa kuuhamisha ubalozi wake mjini Tel Aviv na kuupeleka katika mji mtakatifu wa Quds.
-
Arab League yaionya Marekani dhidi ya kuuhamishia ubalozi wake Quds
Dec 03, 2017 10:56Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imeonya kuwa, kuhamishiwa ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv hadi mji mtukufu wa Quds hakutakuwa na natija nyingine ghairi ya kuibua ghasia na kuvuruga zaidi hali ya mambo.
-
Askari wa Kizayuni wamewakamata Wapalestina 450 mwezi Novemba
Dec 02, 2017 23:17Kituo cha Utafiti wa Wafungwa Wapalestina PPCS kimetangaza kuwa jumla ya Wapalestina 450 walikamatwa na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel mwezi uliopita wa Novemba.
-
ICC yakataa kuifungulia mashtaka Israel kwa kuvamia msafara wa wanaharakati na kuua
Dec 01, 2017 04:01Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC imesema haitaufungulia mashtaka utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na uvamizi uliofanywa na makomandoo wake dhidi ya msafara wa misaada kwa ajili ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza katika maji ya kimataifa mwaka 2010.
-
Rais wa zamani wa Yemen aonyesha nyaraka za ushirikiano wa Saudia na Israel katika vita vya 1967
Dec 01, 2017 01:16Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdullah Saleh ameonyesha nyaraka zinazohusu hatua zilizochukuliwa na Saudi Arabia na Marekani kuiunga mkono Israel katika vita dhidi ya Misri na Syria na vilevile uungaji mkono wa Washington kwa mpango wa kuigawanya Iraq.