Wairani waandamana kulaani uamuzi wa Rais Trump kuhusu Baitul Muqaddas
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i37347-wairani_waandamana_kulaani_uamuzi_wa_rais_trump_kuhusu_baitul_muqaddas
Maelfu ya wananchi wa Iran wameandamana leo baada ya Swala ya Ijumaa katika miji mbalimbali hapa nchini wakilalamikia na kulaani uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kuutambua mji wa Baitul Muqaddas wa Palestina kama mji mkuu wa utawala vamizi wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 08, 2017 11:29 UTC
  • Wairani waandamana kulaani uamuzi wa Rais Trump kuhusu Baitul Muqaddas

Maelfu ya wananchi wa Iran wameandamana leo baada ya Swala ya Ijumaa katika miji mbalimbali hapa nchini wakilalamikia na kulaani uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kuutambua mji wa Baitul Muqaddas wa Palestina kama mji mkuu wa utawala vamizi wa Israel.

Waumini hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu walipiga nara dhidi ya Marekani na utawala haramu wa Israel na kusisitiza juu ya kuendelezwa muqawama na mapambano dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.

Waandamanaji hao walichoma moto bendera ya utawala haramu wa Israel na kutoa nara za kuuhami mji mtakatifu wa Quds kilipo kibla cha kwanza cha Waislamu.

Mjini Tehran pia kama ilivyokuwa katika miji mingine mikubwa ya Isfahan, Tabriz, Mash’had, Shiraz, Qum na kwingine, kulishuhudia maandamano ya waumini baada ya Swala ya Ijumaa ambao mbali na kulaani uamuzi huo wa Trump walitangaza uungaji mkono wao kwa mji wa Baitul Muqaddas na mapambano ya wananchi wa Palestina dhidi ya utawala vamizi wa Israel.

Maandamano ya wananchi wa Tehran wakilalamikia na kulaani uamuzi wa Trump wa kuitangaza Baytul Muqaddas kuwa mji mkuu wa Israel

Waandamanaji wametoa azimio mwishoni mwa maandamano yao lililokuwa na vipengee kadhaa. Sehemu moja ya azimio hilo inasisitiza kwamba, Marekani ni shetani mkubwa na adui nambari moja wa jamii ya mwanadamu na ndio msababishaji mkuu wa vita na ukosefu wa amani Mashariki ya Kati na ulimwenguni kwa ujumla.

Sehemu nyingine ya azimio hilo inasema kuwa, mji wa Quds utabakia milele kuwa ni mji mkuu wa Palestina na kwamba, hatua ya Trump ni kutangaza vita dhidi ya Palestina na ulimwengu wa Kiislamu.