Marekani yatumia VETO kupinga azimio la Quds
https://parstoday.ir/sw/news/world-i37789-marekani_yatumia_veto_kupinga_azimio_la_quds
Licha ya wanachama 14 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuupigia kura ya ndio muswada uliopendekezwa na Misri kuhusu mji mtakatifu wa Baytul Muqaddas, lakini Marekani imeukwamisha muswada huo kwa kura yake ya veto.
(last modified 2026-01-14T11:42:18+00:00 )
Dec 19, 2017 04:26 UTC
  • Marekani yatumia VETO kupinga azimio la Quds

Licha ya wanachama 14 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuupigia kura ya ndio muswada uliopendekezwa na Misri kuhusu mji mtakatifu wa Baytul Muqaddas, lakini Marekani imeukwamisha muswada huo kwa kura yake ya veto.

Muswada wa azimio hilo ulikuwa umesema: Uamuzi au hatua yoyote yenye nia ya kubadilisha utambulisho, hali au muundo wa kijamii wa mji mtakatifu wa Quds, haina athari za kisheria na inabidi ifutwe kwa mujibu wa maazimio ya Umoja wa Mataifa.

Muswada huo aidha ulikuwa imezitaka nchi zote kuheshimu azimio nambari 478 la Baraza la Usalama linalopiga matufuku kufungua ubalozi au ofisi ya ubalozi mdogo katika mji wa Quds na kusichukuliwe hatua yoyote ya kwenda kinyume na azimio hilo.

Donald Trump, rais wa Marekani mwenye chuki za kidini

 

Jana Jumatatu, Misri iliwakabidhi muswada huo wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Hivyo usiku wa kuamika leo Jumanne, baraza hilo likaitisha kikao cha kujadili muswada huo. 

Wanachama wote wa baraza hilo ukitoa Marekani wamepasisha muswada huo na kuitaka Marekani iheshimu maazimio ya Umoja wa Mataifa. Hata hivyo kuweko kura ya kidhulma ya veto kumekwamisha azimio hilo baada ya Marekani kupinga maamuzi ya wengi kwa kura yake hiyo.

Tarehe sita mwezi huu wa Disemba, rais wa Marekani, Donald Trump kwa mara nyingine tena aliwavuruga walimwengu kwa kitendo chake cha kiuadui cha kuitangaza Quds Tukufu yenye Kibla cha Kwanza cha Waislamu kuwa eti ni mji mkuu wa utawala pandikizi wa Kizayuni.

Tangu wakati huo hadi hivi rais huyo wa Marekani analaaniwa kila mahali huku maandamano na upinzani ukishamiri hata kati ya marafiki wa karibu sana wa Marekani kama vile Uingereza.