-
Sasa Uturuki yakata mahusiano yote ya kibiashara na Israel, yafunga anga, bandari kwa sababu ya Ghaza
Aug 30, 2025 02:22Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan ametangaza kuwa nchi hiyo inafunga anga na bandari zake kwa ndege na meli za utawala wa kizayuni wa Israel, na kukata kikamilifu mahusiano yote ya kiuchumi na kibiashara na utawala huo kutokana na vita vyake vya mauaji ya kimbari unavyoendeleza huko Ghaza, Palestina.
-
Uchunguzi: Akthari ya Waisrael wanaamini hakuna Mpalestina yeyote Ghaza 'asiye na hatia'
Aug 28, 2025 02:37Uchunguzi wa maoni uliofanywa na shirika moja katika utawala wa kizayuni wa Israel umefichua kuwa idadi kubwa ya Wayahudi wa Israel wanaamini kwamba hakuna watu wasio na hatia katika Ukanda wa Ghaza.
-
Pigo jingine kwa Mpango wa Abraham; Kwa nini Libya inapinga uhusiano wa kawaida na Israel?
Aug 26, 2025 08:33Serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya imekataa nchi hiyo kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Je, inatosha kwa nchi za Magharibi kulaani kwa maneno matupu jinai za utawala wa Israel?
Aug 25, 2025 23:12Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi 21 za Magharibi kwa pamoja wamelaani uamuzi wa Israel wa kujenga makaazi mapya ya walowezi wa Kizayuni huko Quds Mashariki.
-
Pezeshkian: Migawanyiko kati ya mataifa ya Kiislamu inainufaisha Israel pekee
Aug 25, 2025 07:30Rais wa Iran amesema umoja wa wananchi wa Iran na katika mataifa yote ya Kiislamu ndiyo kinga kuu dhidi ya vitisho vya maadui, akionya kuwa migawanyiko ni kwa maslahi ya Israel pekee.
-
Tangu Agosti 6, jeshi la Israel limebomoa kikamilifu majengo zaidi ya 1,000 ya Mji wa Ghaza
Aug 25, 2025 03:29Shirika la Ulinzi wa Raia la Palestina limetangaza kuwa jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel limebomoa kikamilifu majengo zaidi ya 1,000 katika vitongoji vya Zeitoun na Sabra katika Mji wa Ghaza tangu lilipoanza kuuvamia mji huo mnamo Agosti 6, na hivyo kupelekea mamia ya Wapalestina kunasa chini ya vifusi vya majengo hayo.
-
Hamas yapongeza 'ujasiri' wa mawaziri wa Uholanzi kujiuzulu juu ya Gaza
Aug 24, 2025 23:27Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imepongeza hatua ya kujiuzulu mawaziri kadhaa wa Uholanzi, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Caspar Veldkamp, kujibu hatua ya kukataa kwa serikali yao kuiwekea vikwazo Israel. Hamas imetaja kujiuzulu huko kama uamuzi wa kijasiri na wa kimaadili.
-
Jaribio la Wazayuni la kumuua kigaidi Mkuu wa Majeshi ya Yemen lagonga mwamba
Aug 24, 2025 23:00Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeripoti habari ya kufeli jaribio la utawala haramu wa Israel la kumuua Mkuu wa Majeshi ya Yemen, kwa mara ya pili sasa.
-
Kashfa kubwa ya utawala wa Kizayuni: Israel, kituo kikubwa zaidi cha biashara ya dawa za kulevya barani Ulaya
Aug 23, 2025 06:09Kwa mujibu wa ripoti ya kituo cha runinga cha Israel, Channel 12, Israel inazidi kuwa kitovu kikuu cha biashara ya dawa za kulevya kuelekea katika nchi za Ulaya.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi ajiuzulu, kisa mkwamo wa vikwazo dhidi ya Israel
Aug 23, 2025 03:32Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi, Caspar Veldkamp amejiuzulu baada ya kushindwa kupata uungwaji mkono wa baraza la mawaziri kwa vikwazo zaidi dhidi ya Israel, kutokana na mashambulizi ya kijeshi ya utawala huo wa Kizayuni huko Gaza.