Tsunami ya chuki; Imekuaje Israel imeondokea kuwa utawala unaochukiwa duniani?
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i129198-tsunami_ya_chuki_imekuaje_israel_imeondokea_kuwa_utawala_unaochukiwa_duniani
Katika wiki za hivi karibuni, maafisa na takwimu za Israel zimeelezea mara kwa mara wasiwasi wao juu ya kuongezeka kwa chuki ya kimataifa dhidi ya utawala huo ghasibu.
(last modified 2025-08-06T00:27:25+00:00 )
Aug 06, 2025 00:27 UTC
  • Tsunami ya chuki; Imekuaje Israel imeondokea kuwa utawala unaochukiwa duniani?

Katika wiki za hivi karibuni, maafisa na takwimu za Israel zimeelezea mara kwa mara wasiwasi wao juu ya kuongezeka kwa chuki ya kimataifa dhidi ya utawala huo ghasibu.

Kuongezeka chuki duniani kote kwa utawala wa Kizayuni kumewatia wasiwasi watu na shakhsia mbalimbali katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu. "Barak Sari", mshauri mashuhuri wa mawasiliano ya utawala wa Kizayuni, alitahadharisha kuhusu kuzorota kwa haiba ya utawala huu katika anga ya kimataifa.

Zaidi ya maafisa 550 wa zamani wa utawala wa Kizayuni walituma barua kali kwa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala huo ghasibu wakitahadharisha dhidi ya kuendelea vita vya Gaza bila ya kuwa na lengo la kistratijia la wazi na kueleza kuwa ndio sababu ya kuingia utawala huo katika uvamizi wa muda mrefu na wenye gharama kubwa bila njia ya kutokea.

Matan Vilnai, mkuu wa vuguvugu la "Makamanda wa Usalama wa Israel" alisisitiza katika barua aliyoliandikia baraza la mawaziri la Israel na fikra za walio wengi: "Sera hizi sio tu zitasababisha vita kuwa tata zaidi, lakini pia zitaitenga zaidi Israel kikanda na kimataifa."

Uchunguzi wa maoni wa hivi karibuni wa taasisi kadhaa za Magharibi ambazo pia ni maarufu katika ngazi ya kimataifa, kama vile Taasisi ya Pew, Gallup, YGW na Chuo Kikuu cha Harvard, zote zinaonyesha kutengwa kimataifa Israel, malalamiko ya maoni ya umma na ongezeko kubwa la uharamu na chuki dhidi ya utawala wa Kizayuni, na hii ni moja ya hasara na pigo kubwa zaidi ya utawala huu katika miaka miwili iliyopita.

Kampeni ya kuususia utawala ghasibu wa Israel imeongezeka mno katika mataifa mbalimbali hata barani Ulaya

 

Chuki hiyo ya kimataifa ni kubwa mno kiasi kwamba kwa mujibu wa uchunguzi wa Channel 12 ya utawala wa Kizayuni, asilimia 56 ya wakazi wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu wana wasiwasi kwamba watapoteza uwezekano wa kuondoka katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu kutokana na kuongezeka maandamano ya kimataifa na ukosoaji wa vita vya Gaza.

Swali muhimu ni kwa nini chuki dhidi ya utawala wa Kizayuni imefikia kiwango cha juu zaidi duniani na bado inaendelea kuongezeka?

Sababu muhimu na kuu ya chukizo hiyo ya kimataifa ni kufichuliwa sura ya jinai ya utawala wa Kizayuni mbele ya fikra za waliowengi ulimwenguni. Siasa ya kuwabakisha na njaa watu wa Gaza iliyosababisha vifo vya takriban watu 1,400 kutokana na njaa, ndiyo sababu kuu ya kufichuliwa sura ya kinyama na ya jinai ya utawala huo wa kizayuni.

Watu wa dunia wanaona picha za hali mbaya ya kimwili ya watoto wa Gaza, ambao ama wanakufa kwa njaa au kuhangaika na kifo. Amos Harel, mchambuzi mashuhuri wa gazeti la lugha ya Kiebrania Ha'aretz, aliandika.

Netanyahu alidhani kuwa atafika "pwani salama" mwisho wa kikao cha majira ya joto cha Knesset, lakini njaa huko Gaza ilivuruga mahesabu yote. Hata Donald Trump hakuweza kuzipita  picha chungu za Gaza bila kujali na kutojibu. Harel amesema kuwa, hivi sasa utawala wa Kizayuni unakabiliwa na kuporomoka kwa diplomasia duniani.

Kulingana na Kanali ya 12 ya Televishebni ya Israel, njaa katika Ukanda wa Gaza iko imetawala habari za vyombo vya habari vya ulimwengu leo. Suala hili si tu katika sehemu za habari za washukiwa wakuu, yaani CNN na BBC, lakini leo hii linaonekana katika mitandao yote ya televisheni duniani. Picha za chungu za njaa huko Gaza zinaakisiwa kote kwenye duru za habari na karibu kila raia wa Ulaya huanza siku yake na picha hizi.

Fauka ya hayo, jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni dhidi ya watu wa Gaza na vilevile moyo wa utawala ghasibu wa Israel wa kupenda vita katika eneo la Magharibi mwa Asia ambako raia ndio wahanga wakubwa, kumepelekea kuporomoka thamani na kanuni za kimataifa na utepetevu wa taasisi za kimataifa.

 

Suala hili pia limewakasirisha watu wa dunia kwa sababu wananchi wanaamini kuwa utawala wa Kizayuni umepata kinga chini ya kivuli cha uungaji mkono wa Marekani, jambo ambalo lilmeufanya mfumo wa dunia kushuhudia kuporomoka kwa viwango vya maadili na ongezeko la ufisadi wa kisiasa.

 Kuhusiana na suala hilo, Yair Golan, kiongozi wa chama cha "Democrats" katika utawala wa Kizayuni amekosoa vikali siasa za baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu na kulitaja kuwa ndio sababu kuu ya kuenea chuki dhidi ya Uyahudi na chuki za kimataifa dhidi ya Israel.

Nukta ya mwisho ni kuwa, katika hali ambayo wasi wasi kuhusu ongezeko kubwa la chuki za kimataifa dhidi ya utawala wa Kizayuni ukiambatana na maonyo ya shakhsia na vyombo vya habari katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala huo ghasibu wa kizayuni ametaja sababu ya chuki dhidi ya Israel kuwa ni propaganda na kampeni dhidi ya utawala huo.

Wakosoaji wanaamini kuwa Netanyahu ameigeuza Israel kuwa utawala unaochukiwa duniani ili kusalia madarakani.