Sep 07, 2019 06:20
Tangu yalipofikiwa makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) mwaka 2015, Marekani na utawala wa Kizayuni zimekuwa zikisisitiza kila mara kuwa zinayapinga makubaliano hayo na kutaka yavunjwe. Na katika hatua iliyolenga kufikia lengo hilo, mwezi Mei 2018, Rais Donald Trump wa Marekani alitangza kujitoa nchi yake kwenye makubaliano hayo na kuanza kutekeleza vikwazo vikali ambavyo havijawahi kushuhudiwa dhidi ya Iran.