-
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu asisitiza umuhimu wa kupanda miti
Mar 06, 2018 13:45Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema leo amepanda miti miwili ya matunda katika maadhimisho ya Siki ya Kupanda Miti na Wiki ya Maliasili.
-
Kushindwa maadui mbele ya mhimili wa muqawama kwa mtazamo wa Kiongozi Muadhamu
Mar 02, 2018 04:33Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, Syria leo hii iko katika mstari wa mbele wa muqawama hivyo basi ni jukumu letu kuunga mkono kusimama kidete nchi hiyo na kwamba, Rais wa Syria Bashar al Assad amedhihirika katika sura moja ya mwana muqawama mkubwa na kwamba yupo imara na hakuna shaka yoyote kuhusu Rais Assad; na jambo hilo ni muhimu sana kwa nchi yoyote ile.
-
Kiongozi Muadhamu: Siku ya kusali sala ya jamaa Quds itafika karibuni hivi
Mar 01, 2018 12:10Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, leo Alkhamisi ameonana na kundi la maulamaa wa Syria na kusisitizia wajibu wa kushikamana vilivyo na mambo yanayowaunganisha Waislamu wote. Amesema: Ni matumaini yetu sote tutaiona siku ambayo mtasali sala la jamaa mjini Quds na siku hiyo haiko mbali tena bali itafika karibuni hivi, ni sawa tu kama watu kama sisi tutakuwa bado tupo au hatupo tena.
-
Kiongozi Muadhamu: Vibarua walionyesha uono wa mbali katika matukio ya Mapinduzi na Kujihami Kutakatifu
Feb 26, 2018 11:01Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, kuwaenzi mashahidi wa baadhi ya matabaka kama vile mashahidi vibarua ni jambo lenye thamani maradufu kwa sababu katika matukio yote ya Mapinduzi ya Kiislamu, na kukabiliana na makundi potovu na pia katika zama za kujihami kutakatifu, vibarua nchini Iran walionyesha ghera na uono wa mbali na kujitokeza katika medani.
-
Kiongozi Muadhamu alipongeza taifa kwa kushiriki kwa hamasa kubwa kumbukumbu za Mapinduzi ya Kiislamu
Feb 18, 2018 12:29Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelipongeza taifa la Iran kwa kushiriki kwa hamasa, mshikamano na shauku kubwa katika maadhimisho ya miaka 39 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Kiongozi: Mashia na Masuni nchini wako bega kwa bega katika vipindi vigumu kabisa
Feb 13, 2018 13:19Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kusimama kidete Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mbele ya ujahilia mamboleo pamoja na kuwepo vikwazo na njama zote za kijeshi na kiutamaduni za adui kunatokana na imani na kujitolea mhanga Wairani.
-
Kiongozi Muadhamu awapongeza Wairani kwa ushiriki mkubwa katika maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Feb 12, 2018 01:50Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Jumapili usiku ametoa ujumbe na kuwapongeza wananchi wa Iran kwa kushiriki kwa wingi katika maandamano ya Yawmullah 22 Bahman (11 Februari) ambayo ni siku ya maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Sisitizo la Umoja wa Ulaya la kupatiwa suluhisho mgogoro wa Mashariki ya Kati
Feb 01, 2018 07:50Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini amesema suluhisho la kuundwa nchi mbili kwa ajili ya mgogoro wa Mashariki ya Kati halina chaguo jengine mbadala la kisiasa lenye itibari na la kudumu.
-
Kiongozi: Lengo la Marekani katika kuhamishia Afghanistan magaidi wa ISIS ni kuhalalisha uwepo wake katika eneo
Jan 30, 2018 04:46Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha masikitiko yake makubwa kutokana na kuuawa watu wasio na hatia katika hujuma za hivi karibuni za kigaidi nchini Afganistan na kusema: "Lengo la Marekani katika kuhamishia Afghanistan magaidi wa ISIS (Daesh) ni kuhalalisha uwepo wake katika eneo sambamba na kudhamini usalama wa utawala wa Kizayuni."
-
Ayatullah Khatami: Adui anafanya njama za kulivunja moyo taifa la Iran
Jan 26, 2018 13:21Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa njama za maadui wa Uislamu sasa zimeelekezwa katika mitandao ya kijamii na wanafanya jitihada za kulivunja moyo na kulikosesha matumaini taifa la Iran.