Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu asisitiza umuhimu wa kupanda miti
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i41283-kiongozi_muadhamu_wa_mapinduzi_ya_kiislamu_asisitiza_umuhimu_wa_kupanda_miti
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema leo amepanda miti miwili ya matunda katika maadhimisho ya Siki ya Kupanda Miti na Wiki ya Maliasili.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 06, 2018 17:15 UTC
  • Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu asisitiza umuhimu wa kupanda miti

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema leo amepanda miti miwili ya matunda katika maadhimisho ya Siki ya Kupanda Miti na Wiki ya Maliasili.

Ayatullah Ali Khamenei ameitaja siku na ada ya kupanda miti kuwa ni ada yenye baraka. Ameashiria umuhimu na baraka za mimea, misitu na nyika katika kulinda hali ya hewa, umaridadi na uzuri wa mazingira na katika kuzalisha bidhaa zenye faida kwa mwanadamu na kuwaambia maafisa wa serikali kwamba: Tehran ina mashamba na misitu ambayo kuna baadhi ya watu wanaotaka kuiharibu, lakini kuna ulazima wa kuzuia jambo hilo ambalo lina madhara kwa maisha na hali nzuri ya watu wa mijini.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akipanda mti wa matunda

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amewaagiza maafisa wa taasisi husika kama Wizara ya Jihadi ya Kilimo na Wizara ya Nishati kulipa umuhimu mkubwa suala la usimamizi wa vyanzo vya maji (Watershed Management) kuhusiana na upandaji wa miti na kutengeneza mabustani na akasema: Utekelezaji wa sera hiyo unaweza kuwa sababu ya kuzuia vimbunga vya vumbi na mafuriko.