-
Kim Jong-un ataka kupanuliwa mahusiano na Korea Kusini haraka
Mar 06, 2018 17:10Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini sambamba na kufurahishwa na hatua ya Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini ya kumtuma mjumbe wake maalumu mjini Pyongyang, ametaka kuboreshwa haraka mahusiano ya nchi mbili.
-
Mjumbe wa Rais wa Korea Kusini mjini Pyongyang aanza safari kuimarisha mahusiano zaidi
Mar 05, 2018 08:23Mjumbe maalumu wa Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini amefanya safari nchini Korea Kaskazini ambapo pia amesema kuwa akiwa Pyongyang atajadiliana na viongozi wa nchi hiyo kuhusiana na masuala ya silaha za nyuklia.
-
Pentagon yaonya: Askari 10,000 wa Marekani 'watakufa' vita vikianza tu dhidi ya Korea Kaskazini
Mar 03, 2018 07:56Makamanda wakuu wa jeshi la Marekani wameonya kuwa vita dhidi ya Korea Kaskazini vinaweza kusababisha kuuawa au kujeruhiwa askari wapatao 10,000 wa Marekani katika siku za mwanzoni tu baada ya kuanzishwa vita hivyo, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuliko jumla ya askari 7,000 wa nchi hiyo waliouawa vitani katika nchi za Iraq na Afghanistan.
-
Korea Kaskazini yashangazwa na madai ya Marekani kwamba ilituma silaha za kemikali Syria
Mar 02, 2018 13:54Serikali ya Korea Kaskazini imekadhibisha madai ya viongozi wa Marekani na kadhalika kundi la uchunguzi la Umoja wa Mataifa kwamba ilituma silaha zake za kemikali nchini Syria.
-
Korea Kaskazini: Vikwazo vipya vya Marekani dhidi yetu ni sawa na kututangazia vita
Feb 26, 2018 08:51Korea Kaskazini imesema kuwa, vikwazo vipya vya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya nchi hiyo ni sawa na tangazo la vita dhidi ya Pyongyang.
-
Korea Kusini yakiri kushindwa stratijia za pamoja kati yake na Marekani dhidi ya Korea Kaskazini
Feb 24, 2018 08:04Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini amekiri kufeli stratijia za Washington na Seoul kwa ajili ya kuivua silaha za nyuklia Korea Kaskazini kwa kipindi cha miakka 25 iliyopita.
-
Korea Kaskazini yalaani majaribio ya makombora ya Marekani na Japan
Feb 24, 2018 00:49Serikali ya Korea Kaskazini imetoa taarifa ya kulaani vikali majaribio ya makombora yaliyofanywa na Marekani na Japan.
-
Korea Kusini: Baada ya michuano ya Olimpiki, tutajikita na mazungumzo na Pyongyang
Feb 22, 2018 04:42Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini amesema kuwa, baada ya kumalizika michuano ya sasa ya msimu wa baridi kali inayoendelea huko Pyeongchang, Korea Kusini, Seoul itajikita katika kufanya mazungumzo na Korea Kaskazini kwa ajili ya kutatua maudhui ya silaha za nyuklia za nchi hiyo.
-
Korea Kaskazini ilikataa kukutana kwa siri na viongozi wa Marekani
Feb 21, 2018 07:50Imebainika kuwa, viongozi wa Korea Kaskazini walifuta ghafla mkutano wa faragha uliotatarajiwa kufanyika kati yao na Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence huko nchini Korea Kusini.
-
Korea Kaskazini: Tuhuma bandia za Marekani dhidi yetu zitaigharimu Washington
Feb 16, 2018 07:34Serikali ya Korea Kaskazini imetangaza kwamba, kitendo cha Marekani kuendeleza mashinikizo dhidi yake, kitaigharimu Washington.