Apr 30, 2023 03:34
Nchi 19 za dunia zimeeleza nia yao ya kutaka kujiunga na kundi la BRICS, huku kundi hili, kama taasisi mpya ya kimataifa, likitaka kupanua ushirikiano wa kifedha na kiuchumi kati ya nchi wanachama. BRICS pia imetoa wito wa kufanyika mabadiliko ya miundo ya taasisi za kimataifa, hasa mabadilishano ya kifedha ya kimataifa, na kukabiliana na udhibiiti wa dola ya Marekani katika biashara ya kimataifa.