Jul 25, 2016 08:00 UTC
  • Kongamano la wawekezaji wanawake wa Kenya na Rwanda-Kigali

Rwanda ni mwenyeji wa kongamano la kwanza la ujasiriamali la kujadili changamoto wanazopitia wafanyabiashara wanawake katika kanda ya Afrika Mashariki.

Stephen Ruzibiza, Mkurugenzi Mkuu wa Shirikisho la Sekta ya Kibinafsi nchini Rwanda amesema mkutano huo wa siku tatu unaoanza leo katika hoteli moja mjini Kigali utatoa fursa kwa wafanyabiashara, wajasiriamali na wawekezaji wa kike kutathmini na kuyatafutia ufumbuzi matatizo wanayokumbana nayo katika shughuli zao hizo.

Wanawake wanaojihusisha na biashara za ujenzi na uuzaji wa nyumba, kilimo, kilimo-biashara, utalii, uchukuzi, elimu, kawi, afya na uchimbaji migodi wanashiriki kongamano hilo litakalomalizika Julai 28.

Wafanyabiashara wanawake wa Kenya na Rwanda kwenye mkutano

 

Mary Muthoni, mwenyekiti wa kamati ya wafanyabiashara wanawake katika Jumuiya ya Kitaifa ya Biashara na Viwanda ya Kenya KNCCI amesema wawekezaji hao wa kike wanatapewa mafunzo juu ya masuala ya ushindani na namna ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara wa kikanda chini ya miongozo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Tags