-
Zarif: Ukatili wa Marekani dhidi ya watu wa Iran unaendelezwa kwa ugaidi wa kiuchumi
Jul 04, 2021 08:51Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mohammad Javad Zarif ameashiria namna Marekani ilivyowaua raia wasio na hatia kwa kutungua kwa kombora ndege ya abiria ya Iran Air na kuandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa: "Ukatili wa Marekani dhidi ya watu wa Iran sasa unaendelezwa kupitia ugaidi wa kiuchumi."
-
Jarida la Marekani Hill: Vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran havina taathira
Jul 04, 2021 03:51Jarida la Marekani la Hill limeandika kwamba siasa za Marekani za 'mashinikizo ya juu kabisa' hazijakuwa na matunda yoyote katika utawala wa Donld Trump na wala hazitakuwa na taathira yoyote katika utawala wa rais wa hivi sasa wa Marekani Joe Biden.
-
Wamarekani waendelea kuiba mafuta na maliasili ya Syria
Jul 03, 2021 22:06Wanajeshi vamizi na maharamia wa Marekani wanaendelea kuiba mafuta ya nchi ya Syria waliyoivamia kinyume cha sheria na kuhamisha nishati hiyo nje ya mipaka ya Syria kupitia kaskazini mwa Iraq.
-
Rouhani: Marekani iwajibishwe kwa kutungua ndege ya abiria ya Iran
Jul 03, 2021 08:11Rais Hassan Rouhani wa Iran ameikosoa vikali Marekani kwa kutoomba radhi kwa kushambulia ndege ya abiria ya Jamhuri ya Kiislamu mwaka 1988 katika Ghuba ya Uajemi na kusisitiza kuwa, Washington inapaswa kubebeshwa dhima kwa kuwaunga mkono waliotenda jinai hiyo.
-
Russia yaitaka Marekani iache kuiba rasilimali za Wasyria
Jul 03, 2021 08:10Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema Marekani inapaswa kukomesha tabia yake ya kuiba rasilimali za wananchi wa Syria, na badala yake ipambane na magenge ya kigaidi.
-
Kuhuishwa JCPOA kunategemea maamuzi magumu ya Marekani na Ulaya
Jul 02, 2021 22:15Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema sasa wakati umewadia kwa Marekani na nchi tatu za Ulaya kuchukua maamuzi magumu kwa ajili ya kuanza kufungamana tena kikamilifu na mapatano ya kimataifa ya nyuklia, JCPOA.
-
Russia: Hatua ya Marekani kufunga tovuti za mrengo wa muqawama ni ya kisiasa
Jul 02, 2021 22:13Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amelaani vikali hatua ya serikali ya Marekani ya kufunga tovuti kadhaa za vyombo vya habari vya Iran na mrengo wa muqawama na kusisitiza kuwa, kitendo hicho kimechochewa na misimamo hasi ya kisiasa.
-
Barua za jumuiya 113 za haki za binadamu kwa Biden: Mashambulizi ya droni yanapasa kusitishwa
Jul 01, 2021 22:00Makundi na jumuiya za kutetea haki za binadamu 113 zimemwandikia barua Rais Joe Biden wa Marekani zikitaka kusitishwa mashambulizi ya droni yanayofanywa kinyume cha sheria katika nchi mbalimbali.
-
Kifo cha Rumsfeld, mhandisi mkuu wa vita na mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iraq
Jul 01, 2021 04:23Donald Rumsfeld, waziri wa zamani wa ulinzi wa Marekani ambaye ndiye aliyekuwa mhandisi mkuu wa mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iraq na Afghanistan ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 88.
-
Wanachama wa Baraza la Usalama waitaka Marekani iiondolee Iran vikwazo
Jul 01, 2021 03:11Nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zimeitaka Marekani iiondolee Iran vikwazo vyote kwa mujibu wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.