Al Khazali: Muqawama unasubiri kuondoka kivitendo Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i74394-al_khazali_muqawama_unasubiri_kuondoka_kivitendo_marekani
Katibu Mkuu wa Harakati ya Asa'ib Ahl al-Haq ya nchini Iraq amesisitiza kuwa, kamati ya Kuratibu Muqawama inasubiri kuondoka Marekani kivitendo nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 07, 2021 06:57 UTC
  • Al Khazali: Muqawama unasubiri kuondoka kivitendo Marekani

Katibu Mkuu wa Harakati ya Asa'ib Ahl al-Haq ya nchini Iraq amesisitiza kuwa, kamati ya Kuratibu Muqawama inasubiri kuondoka Marekani kivitendo nchini humo.

Vyombo vya habari vya Iraq leo vmetangaza kuwa, Fuad Hussein Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq na Qassim al Araji Mshauri wa Usalama wa Taifa wa nchi hiyo na Qais al Khazali Katibu Mkuu wa Asa'ib Ahl al-Haq wamekutana na kufanya mazungumzo.   

Pande hizo zimejadili suala la kuondoka wanajeshi vamizi wa Marekani huko Iraq. Katibu Mkuu wa Harakati ya Asa'ib Ahl al-Haq amesisitiza kuwa, Kamati ya Kuratibu Makundi ya Muqawama inasubiri Marekani iondoe kikamilifu vikosi vyake vamizi katika ardhi ya Iraq na kwamba haitaridhika kwa kutolewa taarifa tu. 

Qais al Khazali amesema: Msimamo wa kimaidani wa makundi ya muqawama utategemea hatua za kivitendo na za dhati za kuondoka vikosi hivyo vamizi. 

Ripoti zinasema kuwa, Waziri wa Mambo ya Nje na Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Iraq wamemhakikishia Katibu Mkuu wa Harakati ya Asa'ib Ahl al-Haq kuwa wanajeshi wa Marekani wanakaribia kuondoka Iraq. Mustafa al Kadhimi Waziri Mkuu wa Iraq alitilia mkazo udharura wa kuondoka Iraq wanajeshi wa Marekani hadi kufikia Disemba 31 mwaka huu wakati alikutana na Rais Joe Biden wa nchi hiyo katika ziara ya hivi  karibuni nchini humo.

Joe Biden na Mustafa al Kadhimi mjini Washington