-
Rais Rouhani: Uwepo wa majeshi ya Marekani Asia Magharibi ni pigo kwa usalama na uthabiti wa eneo
Sep 27, 2020 01:12Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, uwepo wa majeshi ya Marekani nchini Iraq, Afghanistan na katika mataifa ya kusini mwa Ghuba ya Uajemi ni pigo kwa amani na uthabiti wa eneo.
-
Kurejea kwenye mapatano ya nyuklia ya JCPOA, hatua ya kwanza inayopasa kuchukuliwa na Marekani
Sep 27, 2020 00:38Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akiyataja mapatano ya nyuklia ya JCPOA kuwa ndiyo mapatano mabaya zaidi kwa nchi yake na hatimaye mwezi Mei mwaka 2018 aliiondoa nchi hiyo kwenye mapatano hayo na kuiwekea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vikwazo vikali. Hivi sasa Joe Biden mgombea wa kiti cha urais wa chama cha Democratic huko Marekani amesema iwapo atashinda uchaguzi huo wa mwezi Novemba mwaka huu atairejesha Marekani katika mapatano hayo ya JCPOA.
-
Rouhani: White House ni mhusika wa jinai zote dhidi ya taifa la Iran
Sep 26, 2020 08:49Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Ikulu ya White House ya Marekani ndilo chimbuko la jinai zote dhidi ya binadamu, mashinikizo na vikwazo visivyo vya kiutu dhidi ya wananchi wa Iran.
-
Siri ya Netanyahu na mkewe kubeba nguo chafu Marekani ili zikafuliwe bure hotelini yafichuka
Sep 26, 2020 04:22Gazeti la Washington Post limefichua kuwa, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu amekuwa na mtindo wa kubeba nguo chafu anapokuwa katika ziara rasmi nchini Marekani ili zikafuliwe kwa gharama za serikali ya nchi hiyo badala ya yeye mwenyewe kulipia gharama za ufuaji.
-
Pompeo atishia kufunga ubalozi wa Marekani nchini Iraq endapo utaendelea kushambuliwa
Sep 26, 2020 04:21Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo ametoa vitisho kwa viongozi wa Iraq kwamba Washington inaweza kuamua kuufunga ubalozi wake ulioko mjini Baghdad.
-
Sisitizo la maseneta wa Marekani, vikwazo vya Trump kwa Iran vimeshindwa
Sep 26, 2020 02:25Serikali ya Donald Trump nchini Marekani na hatua yake ya kujitoa kijeuri katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA hapo mwezi Mei 2018 kama sehemu ya siasa zake za kuiwekea Iran vikwazo vya kiwango cha ambavyo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijawahi kuwekewa mfano wake katika historia yake yote, imezidi kufeli kiasi kwamba sasa maseneta wa chama cha Democrats wanamshutumu na kumlaumu vikali Trump kwa siasa zake mbovu.
-
Newsweek: Serikali ya Trump inaficha ugaidi wa ndani unaofanywa na wazungu
Sep 25, 2020 04:53Jarida la kila wiki la Newsweek nchini Marekani limechapisha makala ya mshauri wa zamani wa Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo (Pentagon) Jasmine el Gamal ambaye amesema kuwa licha ya kupita mwaka mmoja sasa tangu Wizara ya Usalama wa Ndani ya Marekani iliyoanzishwa baada ya mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 kutangaza azma yake ya kupambana na ugaidi wa ndani na vitisho vya wazungu wenye misimamo mikali, lakini uchunguzi unaonesha kuwa, wizara hiyo haijachukua hatua yoyote katika uwanja huo.
-
HAMAS: Mpango wa Israel wa kupora ardhi za Ukingo wa Magharibi utagonga mwamba
Sep 24, 2020 08:29Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, njama za Marekani na utawala haramu wa Israel za kutaka kutwaa ardhi zaidi katika Ukingo wa Magharibi na kuziunganisha na ardhi nyingine zilizoghusubiwa za Palestina zitashindwa na kugonga ukuta.
-
Mivutano baina ya Marekani na China yashadidi baada ya hotuba ya Trump katika Umoja wa Mataifa
Sep 24, 2020 04:40Katika hotuba yake ya mwisho kwenye ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika kipindi chake cha kwanza cha urais wa Marekani, Donald Trump amejikita zaidi katika masuala ya China na Iran na kudai kuwa, Marekani imejiondoa katika makubaliano mabaya sana ya nyuklia ya JCPOA na imeiwekea Iran vikwazo vya kulema.
-
Venezuela yaunda kikosi maalumu cha makomando kukabiliana na chokochoko za Marekani
Sep 23, 2020 23:12Rais Nicolas Maduro wa Venezuela ameukosoa vikali ujambazi na umafia unaofanywa na serikali ya Marekani dhidi ya nchi yake na ametangaza habari ya kuundwa kikosi maalumu cha makomando cha kupambana na vitendo vya kiharibifu vya Marekani.