-
Polisi wa Marekani waendeleza jinai zao, mara hii wamuua Mmarekani mwenye asili ya Latini asiye na silaha
Jun 05, 2020 22:27Katika jinai mpya zinazochochewa na mitazamo ya kibaguzi, polisi wa Marekani, wamemuua raia wa nchi hiyo mwenye asili ya Amerika ya Latini ambaye hakuwa na silaha wala ulinzi wowote.
-
Jitihada mpya za Marekani kwa ajili ya kurefusha vikwazo vya silaha dhidi ya Iran
Jun 05, 2020 22:23Moja kati ya vipengee muhimu vya mapatano ya nyuklia ya maarufu kwa kifupi ka jina la JCPOA ni azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lina kipengee kuhusu kufutwa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran miaka mitano baada ya kuanza kutekelezwa mapatano hayo.
-
Pelosi naye aiponda Israel na Muamala wa Karne wa Donad Trump
Jun 05, 2020 07:29Spika wa Kongresi ya Marekani ametahadharisha kwamba, mpango wa Israel wa kutaka kutwaa ardhi nyingine ya Palestina ya Ukingo wa Magharibi (West Bank) utadhoofisha sera za vyama viwili vikuu vya Marekani, Democratic na Republican, za kuiunga mkono Tel Aviv.
-
Malalamiko ya UN dhidi ya ubaguzi wa rangi wa kitaasisi nchini Marekani
Jun 05, 2020 01:27Ubaguzi wa rangi na kizazi na ukandamizaji uliochupa mipaka dhidi ya watu wasio wazungu hasa wenye asili ya Afrika huko Marekani una historia ndefu na ulianza tangu ilipoasisiwa nchi hiyo karne tatu zilizopita. Ubaguzi huo daima umekuwa ni sifa inayochukiza ya jamii ya Marekani. Licha ya Wamarekani wenye asili ya Afrika kuendesha mapambano makali ya kupigania haki zao, lakini hadi leo hii wanaendelea kuwa wahanga wa ubaguzi, ukatili na ukandamizaji usio na kifani.
-
Waziri wa Ulinzi China: Uhasama wa Marekani na China umeingia kipindi hatari
Jun 04, 2020 21:55Waziri wa Ulinzi wa China amesema uhasama wa kistratijia wa nchi yake na Marekani umeingia kipindi hatari baada ya Washington kukithirisha sera zake za 'kuikandamiza na kukabiliana' na China baada ya janga la COVID-19 kuikumba dunia.
-
Obama ataka mageuzi Marekani, Pelosi ajiunga na waandamanaji dhidi ya ubaguzi wa rangi
Jun 04, 2020 08:16Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama ametoa wito wa kufanyika marekebisho katika mfumo wa jeshi la polisi la nchi hiyo na kusisitiza kuwa, waandamanaji wanaopinga ubaguzi wa rangi wanapaswa kuwanyima utulivu wanaoshikilia madaraka.
-
Wasiwasi wa Pentagon na hata Republican kwa hatua ya Trump ya kutumia wanajeshi kukandamiza waandamanaji Marekani
Jun 04, 2020 08:11Maandamano makubwa ambayo hayajawahi kutokea mfano wake huko Marekani yamemtia kiwewe na kumuweka kwenye hali ngumu rais wa nchi hiyo mwenye majigambo na majivuno mengi, Donald Trump na kumfanya atoe amri ya kutumiwa jeshi, suala ambalo limelalamikiwa na Wizara ya Ulinzi, lakini hata wanachama wenzake ndani ya chama cha Republican nao hawakubaliani na uamuzi wake wa kutumia nguvu za kijeshi kukandamiza waandamanaji.
-
Hata 'Mbwa Kichaa' akosoa mienendo ya Trump; zaidi ya 10,000 wakamatwa katika maandamano Marekani
Jun 04, 2020 03:25Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani, James Mattis maarufu kwa jina la "Mbwa Kichaa" ametangaza kuwaunga mkono wananchi wa Marekani wanaondamana kulaani ubaguzi wa rangi na mienendo ya kikatili ya polisi ya Marekani hususan dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika.
-
Kiongozi Muadhamu atilia mkazo udharura wa kujifunza fikra za hayati Imam Khomeini
Jun 04, 2020 03:09Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema jana alihutubia taifa kwa njia ya televisheni kwa mnasaba wa kukumbuka siku aliyoaga dunia hayati Imam Ruhullah Khomeini, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akisema kuwa kutaka mabadiliko, kuwa na ari ya kufanya mabadiliko na kuyafanya mageuzi ni miongoni mwa sifa muhimu za hayati Imam Khomeini.
-
Gambia yataka uchunguzi wa mauaji ya mtoto wa mwanadiplomasia nchini Marekani
Jun 04, 2020 00:16Serikali ya Gambia imeitaka Marekani ianzishe uchunguzi mara moja wa mauaji ya mtoto wa kiume wa mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa nchi hiyo ya Kiafrika katika jiji la Atlanta, jimboni Georgia.