-
Kukiri jamii ya ujasusi ya Marekani kwamba Hamas haijashindwa huko Gaza
Mar 27, 2025 22:57Ripoti kuhusu vitisho ambayo hutolewa kila mwaka na jamii ya masuala ya ujasusi ya Marekani imekiri kwamba kundi la muqawama wa Palestina la Hamas huko Gaza halijashindwa bado na kwamba linaendelea kudumisha nguvu, wapiganaji na miundombinu yake.
-
Cuba: Uhamiaji umekuwa biashara kwa Marekani
Mar 27, 2025 22:56Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba amepinga viza ya kadi ya dhahabu ya kupewa makazi mkabawa wa dola milioni tano ya Marekani, na kuituhumu serikali ya Trump kwa kutumia suala la uhamiaji kama biashara, kwa kuuza nyumba na kuwafukuza wahamiaji haramu.
-
Kutozwa ushuru wa asilimia 25 na Marekani kwa nchi zinazonunua mafuta ya Venezuela
Mar 27, 2025 02:19Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza kutoza ushuru wa asilimia 25 kwa biashara yoyote na nchi zinazonunua mafuta na gesi ya Venezuela. Ameelezea ushuru huu kama jibu la kutumwa Marekani wanachama wa genge la uhalifu la "Tren de Aragua".
-
Upinzani wa serikali ya Trump dhidi ya hatua za Ulaya za kupinga Russia
Mar 25, 2025 23:09Baada ya kuchaguliwa tena kwa mara ya pili Rais Donald Trump wa Marekani sasa amegeukia mazungumzo ya moja kwa moja na Russia nchini Saudi Arabia ili kutimiza ahadi aliyotoa ya kuhitimisha vita huko Ukraine ambapo jumbe za Marekani na Russia tayari zimefanya duru ya pili ya mazungumzo huko Riyadh Saudi Arabia kuhusiana na suala hilo.
-
Mapatano mapya ya nchi za Umoja wa Ulaya dhidi ya Russia
Mar 24, 2025 07:04Kwa kutilia maanani jaribio la utawala wa Trump la kuanzisha usitishaji vita nchini Ukraine kwa kuilazimisha ikubali masharti yaliyowekwa na Russia na upinzani wa nchi za Umoja wa Ulaya dhidi ya suala hili, na kwa upande mwingine madai ya baadhi ya viongozi wa Ulaya kuhusu vitisho vya Russia dhidi ya bara hilo, nchi hizo sasa zimechukua hatua mpya kwa ajili ya kukabiliana na Moscow.
-
Balozi wa Trump: Russia haitaki kushambulia Ulaya
Mar 22, 2025 23:10Mjumbe maalum wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati (Asia Magharibi), Steve Witkoff amepuuzilia mbali madai kwamba Russia ina nia ya kuzivamia nchi nyingine za Ulaya, akisisitiza kuwa hofu hizo ni za "kipuuzi".
-
Ujumbe unaogongana wa Marekani kwa Iran: Salamu za Nowruz zilizowekwa viungo vya kushadidisha vikwazo
Mar 22, 2025 22:52Katika siku ya kwanza ya mwaka mpya wa Kiirani wa 1404 Hijiria Shamsia, Wizara ya Fedha ya Marekani imeiwekea Iran vikwazo vipya, ambavyo vinalenga idara kadhaa, meli na watu binafsi, huku Rais Donald Trump wa nchi hiyo, akidai kuwatakia Wairani heri ya mwaka mpya. Kwa maneno mengine ni kuwa, salamu za Nowruz za Wamarekani kwa Wairani zimewekwa viungo vya kushadidisha vikwazo na mashinikizo dhidi yao.
-
New York Times: Marekani haitaweza kuishinda Yemen
Mar 22, 2025 03:30New York Times limeandika kuwa Marekani haitaweza kutoa pigo kwa Yemen katika mashambulizi yake ya kichokozi dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Moto mpya wa vita wawashwa na utawala wa Kizayuni huko Gaza kwa msaada wa Marekani
Mar 20, 2025 06:22Kwa kukiuka makubaliano ya usitishaji vita huko Ghaza yaliyoanza kutekelezwa tarehe 19 Januari, utawala wa Kizayuni umeanzisha tena vita vya umwagaji damu dhidi ya eneo hilo lililoharibiwa na vita, kwa kufanya mashambulizi makubwa ya kinyama ambayo yamesababisha mauaji ya mamia ya mashahidi wa Kipalestina na kujeruhi wengine wengi katika ukanda huo.
-
Onyo la Iran kwa Marekani kuhusu matokeo mabaya ya uchokozi wa aina yoyote
Mar 19, 2025 23:04Amir Saeed Irvani, Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa alitahadharisha katika barua yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu kwamba, hatua zozote za kichokozi zitakazofanywa na Marekani zitakuwa na matokeo mabaya na hatari mno.