Balozi wa Trump: Russia haitaki kushambulia Ulaya
Mjumbe maalum wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati (Asia Magharibi), Steve Witkoff amepuuzilia mbali madai kwamba Russia ina nia ya kuzivamia nchi nyingine za Ulaya, akisisitiza kuwa hofu hizo ni za "kipuuzi".
Witkoff amesema hayo katika mahojiano na mwandishi wa habari wa Marekani, Tucker Carlson, kama ilivyoropitiwa na shirika la habari la Russia Today jana Jumamosi.
Alipoulizwa juu ya tamko la Uingereza kwamba iko tayari kutuma wanajeshi Ukraine kusaidia kuhakikisha makubaliano ya amani yanayoweza kusainiwa kati ya Moscow na Kiev, Witkoff amependekeza kwamba, wabunge wa Uingereza wanataka kuwa "kama Winston Churchill," ambaye alionya kwamba "Warusi wataenda kuandamana kote Ulaya."
Alipoulizwa na Carlson kama anadhani Russia inataka kuvamia na kushambulia nchi nyingine za Ulaya, Witkoff amejibu kwa kusema: "100% hapana, nadhani huo ni ujinga."
Mwanadiplomasia huyo wa Marekani ameendelea kusema: Tuna kitu kinachoitwa NATO ambacho hatukuwa nacho katika Vita vya Pili vya Dunia."
Witkoff ameeleza kuwa, Russia tayari imefikia malengo yake katika mzozo huo (wa Ukraine) na kwa msingi huo hadhani kana ina azma ya kushambulia nchi nyingine ya Ulaya. "Wamerejesha mikononi mwao mikoa hii mitano. Wana Crimea, na wamepata wanachotaka. Kwa nini wanahitaji zaidi?"