-
Makahama ya Misri yaakhirisha hukumu ya watuhumiwa wa Medani ya Rabia
Jun 30, 2018 11:46Mahakama ya Jinai ya Cairo leo Jumamosi imeamua kuakhirisha hukumu ya mwisho dhidi ya watu 739 walioshiriki katika maandamano ya mwaka 2013 ambayo yalisambaratishwa kwa mabavu na vyombo vya usalama na kusababisha moja kati ya mauaji makubwa zaidi ya raia katika historia ya sasa ya nchi hiyo.
-
"Saudia iliipa hongo timu ya taifa ya Misri ikubali kuifunga kombe la dunia" - Mwandishi
Jun 27, 2018 03:25Mwandishi mmoja wa Misri amelalamika kuwa serikali ya nchi yake ilipokea rushwa na hongo kutoka kwa Saudi Arabia na kuilazimisha timu ya taifa ya nchi hiyo ikubali kufungwa na Saudia katika mashindano ya fainali za kombe la dunia yanayoendelea nchini Russia hivi sasa.
-
Hali ya hatari yarefushwa nchini Misri
Jun 24, 2018 22:24Bunge la Misri kwa mara ya nne limeongeza muda wa hali ya hatari kwa miezi mingine mitatu.
-
Harakati ya mitandao ya kijamii ya kumtaka Rais Sisi wa Misri aondoke madarakani
Jun 23, 2018 20:44Kufuatia kuendelea kuwa mbaya mgogoro wa kiuchumi na kisiasa nchini Misri, wananchi ambao wanakandamizwa sasa wameamua kutumia mitandao ya kijamii hasa Twitter kulalamikia utawala wa Rais Abdel Fatah el Sisi huku wengi wakimtaka aondoke madarakani.
-
Misri yachukua hatua kali za usalama kukabiliana na malalamiko ya wananchi
Jun 17, 2018 22:36Serikali ya Misri imechukua hatua kali za kiusalama kwa ajili ya kukabiliana na malalamiko ya wananchi baada ya kuzidishwa bei ya nishati nchini humo.
-
Jumatatu tarehe 18 Juni, 2018
Jun 17, 2018 22:05Leo ni Jumatatu tarehe 4 Shawwal 1439 Hijria sawa na Juni 18, 2018.
-
Al Azhar yalaani wito wa kufutwa aya za Qur'ani
Jun 12, 2018 03:47Sheikh Mkuu wa Al Azhar nchini Misri, Ahmad Tayyib amekosoa vikali wito uliotolewa na kundi la eti wasomi na wanasiasa wa Ufaransa wa kufutwa aya za Qur'ani tukufu.
-
Kiongozi wa HAMAS: Iran ni nchi muhimu na mhimili wa msingi katika eneo
Jun 11, 2018 10:30Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ameuenzi na kuusifu mchango wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuihami na kuiunga mkono Palestina na kusisitiza kwamba: Hamas haiungi mkono mhimili wowote wa Kiarabu au wa kieneo dhidi ya mhimili mwengine.
-
Watu wanne wauawa katika mapigano ya jeshi la Misri na magaidi Sinai Kaskazini
Jun 11, 2018 09:36Duru za habari za Misri zimetangaza habari ya kuuawa watu wanne katika mapigano yaliyozouka baina ya jeshi la Misri na makundi yenye silaha katika mkoa wa Sinai Kaskazini.
-
Misri na Imarati zapinga kufanyika uchaguzi wa Rais na Bunge nchini Libya
Jun 09, 2018 22:19Misri na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) zimeelezea kutofurahishwa kwao na maamuzi wa mkutano wa mjini Paris Ufaransa kuhusiana na Libya na kusema kuwa zinapinga uchaguzi wa Rais na Bunge uliopangwa kufanyika nchini humo tarehe 10 Disemba mwaka huu.