-
Hujjatul Islam Kazem Seddiqi : Muqawama wa Lebanon ulivunja pembe ya Wamarekani
May 27, 2022 11:10Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran ametoa pongezi kwa mnasaba wa maadhimisho ya miaka 22 ya ushindi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon dhidi Wazayuni na kusema, Wazayuni walionja ladha chungu ya kwanza ya kushindwa baada ya kuondoka kwa madhila huko kusini mwa Lebanon.
-
Nasrallah: Watu wa Lebanon hawapingi Hizbullah kumiliki silaha
May 10, 2022 04:33Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah ameashiria uchunguzi wa maoni wa hivi karibuni na kusema tatizo la waliowengi nchini Lebanon si silaha za Hizbullah au Muqawama bali ni hali ya maisha.
-
Rais wa Iran: Mustakabali wa eneo hili utaamuliwa na wanamapambano, sio meza ya mazungumzo
May 09, 2022 03:13Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kitakachoamua mustakabali wa eneo la Asia Magharibi na Palestina sio meza za mazungumzo na makubaliano kama yale ya "Oslo", "Camp David" na" Muamala wa Karne", bali muqawama na mapambano ya mataifa ndiyo yatakayoamua na kupanga utaratibu mpya wa kanda hiyo.
-
Sisitizo la Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu la kupanuliwa muqawama kote Palestina
Apr 30, 2022 11:29Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu jana Ijumaa alihutubu kwa njia ya televisheni kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds ambapo alitaja dalili kadhaa zenye kutia matumaini kuhusu mustakbali tofauti kwa maslahi ya wananchi wa Palestina ikiwemo kupanuliwa uwanja wa mapambano katika ardhi yote ya Palestina na mkabala wake, kudhoofika utawala ghasibu wa Kizayuni na muungaji wake mkono mkuu yaani Marekani.
-
Muqawama wa kutumia silaha; aina bora kabisa ya kupambana na utawala wa Kizayuni
Apr 28, 2022 02:42Makundi ya muqawama ya Palestina yametoa tamko la pamoja katika wakati huu wa kukaribia mno Siku ya Kimataifa ya Quds ambayo ni kesho Ijumaa tarehe 29 Aprili 2022 na mbali na kuashiria jinai za utawala wa Kizayuni yamesema kwamba, mapambano ya kutumia silaha ndio muqawama bora kabisa wa kukabiliana na utawala wa Kizayuni.
-
Sisitizo la Iran la kurudishwa amani ya kudumu katika eneo kwa kuondolewa ukaliwaji mabavu wa ardhi za Palestina
Apr 22, 2022 08:16Hussein Amir Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa amani ya kudumu katika eneo la Asia Magharibi itapatikana tu kwa kuondolewa kikamilifu ukaliwaji mabavu wa ardhi za Palestina, kurejea wakimbizi wote katika ardhi zao za jadi na kuainishwa mfumo wa utawala wa baadaye wa Palestina kwa msingi wa kura ya maoni pamoja na kuundwa serikali huru katika ardhi hizo.
-
Siku ya Muqawama katika Mwezi wa Ramadhani; irada ya Wapalestina ya kukabiliana na jinai za Wazayuni
Apr 16, 2022 09:34Siku ya Ijumaa alfajiri, askari wa utawala haramu wa Israel waliwashambulia Wapalestina ndani ya Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds (Jerusalem) ambapo zaidi ya waumini 150 wamejeruhiwa. Jinai hiyo imewapa Wapalestina irada ya kuimarisha mapambano yao dhidi ya adui Mzayuni mtenda jinai.
-
Spika wa Lebanon: Iran ndio chimbuko kuu la muqawama katika eneo
Mar 25, 2022 14:23Spika wa Bunge la Lebanon ameitaja Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama chanzo kikuu cha harakati za muqawama katika eneo la Asia Magharibi, zilizoipa ilhamu kambi ya muqawama kote duniani.
-
Makundi ya muqawama yailaani Australia kwa kuiita HAMAS kundi la kigaidi
Feb 19, 2022 02:56Makundi ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina yamekosoa vikali kitendo cha Australia cha kuitambua harakati ya muqawama ya HAMAS kuwa ni kundi la kigaidi.
-
Nasrullah: Hizbullah ina uwezo wa kuunda ndege zisizo na rubani
Feb 17, 2022 03:18Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah amesema harakati hiyo sasa inajiundia ndege zisizo na rubani au drone na makombora yenye uwezo wa kulenga shabaha kwa umakini mkubwa.