-
Rais wa Nigeria athibitisha kuuawa afisa wa ngazi ya juu wa jeshi
Nov 19, 2025 08:54Rais wa Nigeria amethibitisha kuwa Brigedia jenerali Musa Uba ameuawa na kundi la kigaidi akiwa matekani. Mauaji hayo yamefanywa siku chache baada ya afisa huyo wa ngazi ya juu wa jeshi la Nigeria kutekwa nyara na wanamgambo wa kundi la ISWAP kufuatia shambulio la kuvizia kaskazini mashariki mwa Jimbo la Borno ambalo pia liliwaua wanajeshi wanne.
-
Mkuu wa jeshi la Nigeria aagiza kutafutwa usiku na mchana mabinti wa shule waliotekwa nyara
Nov 18, 2025 22:53Jenerali wa ngazi ya juu wa jeshi la Nigeria ameviagiza vikosi vya jeshi hilo kuendesha msako wa "usiku na mchana" ili kuwanusuru mabinti 25 wa shule waliotekwa nyara kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo.
-
Magaidi 200 wauawa katika mapigano kati ya makundi hasimu ya kigaidi nchini Nigeria
Nov 10, 2025 23:26Mapigano kati ya makundi hasimu ya kigaidi kaskazini mashariki mwa Nigeria yamesababisha vifo vya magaidi wasiopungua 200 katika eneo la Ziwa Chad.
-
Waislamu na Wakristo wa Nigeria wapinga vitisho vya Trump
Nov 04, 2025 23:41Waislamu na Wakristo wa Nigeria wamesisitiza kuishi pamoja kwa amani na maelewano na kusema kuwa vitisho vya Rais wa Marekani dhidi ya nchi hiyo havikubaliki.
-
Nigeria yapinga vikali vitisho vya Trump, yasema mamlaka yake ya kujitawala hayajadiliwi
Nov 02, 2025 07:11Serikali ya Nigeria imepinga vikali uingiliaji wowote wa kigeni katika mambo ya ndani ya nchi hiyo ikisisitiza kwamba "mamlaka ya kitaifa hayawezi kujadiliwa," na kwamba inachunguza matukio ya hivi karibuni na kuwafuatilia wale wote waliohusika.
-
Trump atishia kuishambulia kijeshi Nigeria kwa tuhuma za alichokiita 'kuuliwa raia Wakristo wapendwa'
Nov 02, 2025 02:56Rais Donald Trump wa Marekani ametishia kufanya mashambulizi ya kijeshi ndani ya ardhi ya Nigeria kutoa mjibizo kwa alichodai kuwa ni ukatili wanaofanyiwa Wakristo, akisema ameiagiza Wizara yake ya Vita aliyoipa jina hilo jipya hivi karibuni "kujiandaa kwa hatua zinazowezekana" kuchukuliwa.
-
Harakati ya Kiislamu ya Nigeria yataka kuachiliwa wanaharakati wa Sumud
Oct 10, 2025 02:55Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imelaani kitendo cha utawala wa Kizayuni cha kuendelea kuwashikilia wanaharakati wa msafara wa kimataifa wa meli nyingi wa Sumud uliokuwa ukielekea Ukanda wa Gaza, na kutaka kuachiwa mara moja kwa raia wa Nigeria na wa mataifa mengine waliotekwa nyara na kuzuiliwa na askari wa majini wa Kizayuni.
-
Wanigeria waandamana kulaani shambulio la Israel dhidi ya msafara wa Sumud
Oct 04, 2025 02:34Waislamu kote nchini Nigeria waliingia barabarani baada ya Swala ya Ijumaa hapo jana kulaani shambulio la Israel dhidi ya msafara wa kimataifa wa Sumud, wenye makumi ya meli zinazoelekea katika Ukanda wa Gaza.
-
Jumatano, Oktoba Mosi, 2025
Sep 30, 2025 23:01Leo ni Jumatano tarehe 8 Mfunguo Saba Rabiul-Thani 1447 Hijria Qamaria, sawa na tarehe 9 Mehr mwaka 1404 Hijria Shamsia, inayosadifiana na tarehe Mosi Oktoba 2025 Miladia.
-
Wafanyakazi wa sekta ya mafuta Nigeria waendelea na mgomo wakipinga kupunguzwa wafanyakazi katika kiwanda cha Dangote
Sep 30, 2025 08:28Ofisi za idara ya Udhbiti wa Mafuta na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Nigeria zimefungwa kutokana na mgomo wa kitaifa ulioanzishwa na jumuiya ya wafanyakazi wa sekta ya mafuta baada ya kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote kuwafuta kazi zaidi ya wafanyakazi 800.