Pars Today
Watu wenye silaha wameua abiria wasiopungua 11 katika matukio mawili tofauti yaliyojiri kusini magharibi mwa Pakistan.
Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, kustawishwa uhusiano wa Iran na Pakistan hakufurahishi madola ya kibeberu na kwa hivyo yanazusha fitna ili kuleta mpasuko kati ya mataifa hayo mawili na nchi hizo mbili za Kiislamu.
Kamanda wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) amesema kuwa, hadi hivi sasa magaidi 15 wameshaangamizwa katika operesheni za kuzima mashambulizi matatu ya kigaidi yaliyofanywa na magaidi hao kusini mashariki mwa Iran.
Musadik Masood Malik, Waziri wa Mafuta wa Pakistan amesema kuwa nchi yake inahitajia mno gesi ya Iran na kwamba msimamo wa Islamabad uko wazi kuwa, kukamilishwa mradi wa kupelekwa gesi ya Iran nchini Pakistan ni jambo la dharura.
Leo ni Jumamosi 12 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani 1445 Hijreia mwafaka na 23 Machi 2024.
Kiongozi wa kundi la kigaidi la "Jaish al-Dhulm" ameuawa katika shambulio la askari usalama wa Iran.
Tume ya Uchaguzi ya Pakistani imetangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa bunge nchini humo, na wagombea huru wenye mfungamano na chama cha Tehreek-e-Insaf cha Imran Khan wamenyakua viti 101.
Wapakistani wapatao milioni 128 waliotimiza masharti leo wameelekea kwenye vituo vya kupigia kura katika uchaguzi mkuu muhimu wa kuchagua serikali mpya itakayoongoza nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo, huku usalama ukiimarishwa kwa kuchukuliwa hatua kadhaa ikiwemo kusitishwa huduma za simu za mkononi na mtandao wa intaneti licha ya kuripotiwa matukio kadhaa ya mauaji.
Maafisa husika wa Afya wameripoti kutoka Pakistan kuwa watoto zaidi ya 19,000 katika jimbo la Punjab kaskazini mashariki mwa nchi hiyo wamegunduliwa kuugua maradhi ya homa ya mapafu yaani nimonia (Pneumonia) baada ya kufanyiwa vipimo katika kipindi cha mwezi mmoja wa karibuni.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, juhudi zinafanyika kuhakikisha kwamba, mipaka ya nchi yake na Pakistan inabadilika na kuwa ya kiuchumi, amani na urafiki.