Jun 08, 2019 02:15
Mvutano unaoendelea kati ya Qatar na nchi nyingine nne za Kiarabu za Saudi Arabia, Bahrain, Imarati na Misri, ambao ulianza tarehe 5 Juni mwaka 2017, uliingia rasmi katika mwaka wake wa tatu hapo tarehe 5 mwezi Juni mwaka huu, katika hali ambayo hakuna dalili zozote zinazoonyesha kwamba mvutano huo utamalizika hivi karibuni.