-
Zaidi ya mamluki 100 wa Saudia waangamizwa ndani ya siku tatu nchini Yemen
Mar 31, 2017 02:33Wizara ya Ulinzi nchini Yemen imetangaza kuwa, zaidi ya mamluki 100 wa utawala wa Aal Saud wameuawa katika mashambulizi ya makombora na mizinga iliyovurumishwa na jeshi hilo katika kipindi cha siku tatu zilizopita.
-
Maandamano Sana'a kulaani vita vya Saudia dhidi ya Yemen
Mar 26, 2017 10:27Mamilioni ya wananchi wa Yemen wameandamana leo katika mji mkuu Sana'a na maeneo mengine nchini humo katika mwanzo wa mwaka wa tatu tokea Saudia ianzishe vita vyake vya kinyama dhidi ya nchi hiyo ambavyo vimesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine wengi kupoteza makazi yao.
-
Ufaransa inaiuzia Saudia silaha za kuwaulia raia waliodhulumiwa wa Yemen
Mar 21, 2017 11:31Rais wa Ufaransa ametoa kibali cha kuuzia silaha utawala wa Aal Saud na hivyo kuuchochea waziwazi utawala huo kuendelea kuwauwa wananchi wa wasio na ulinzi na waliodhulumika wa Yemen.
-
Familia za wahanga wa Septemba 11, zafungua mashtaka dhidi ya Saudi Arabia
Mar 21, 2017 10:01Familia za wahanga waliopoteza maisha katika mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani wamefungua mashtaka dhidi ya utawala wa kifalme wa Saudi Arabia.
-
Jeshi la Yemen: Sasa Saudia ijiandae kwa operesheni mpya ndani ya nchi hiyo
Mar 21, 2017 04:18Naibu Msemaji wa Jeshi la Yemen, ameionya Saudi Arabia kwamba, ikiwa itaendelea kushambulia bandari za Yemen, basi jeshi la nchi hiyo na harakati ya wananchi ya Answarullah, zitafanya operesheni ndani ya ardhi ya Saudia.
-
Waziri Mkuu wa Somalia: Saudia, mhusika wa mauaji ya wakimbizi wa Kisomali
Mar 20, 2017 11:38Serikali ya Somalia imesema kuwa utawala wa Saudi Arabia ndio uliohusika na mauaji ya wakimbizi wa nchi hiyo katika maji ya Yemen.
-
Saudia yaitaka UN isimamie bandari ya Yemen baada ya kuua kikatili Wasomali 44
Mar 20, 2017 04:31Muungano vamizi wa kijeshi wa Saudi Arabia nchini Yemen umeutaka Umoja wa Mataifa uchukue udhibiti wa bandari ya Hudaydah baada ya helikopta ya Aal-Saud aina ya Apache kufanya shambulio la kikatili dhidi ya boti ya wakimbizi karibu na Lango Bahari la Bab al-Mandab, pwani ya Yemen na kuua makumi ya raia wa Somalia.
-
Uchunguzi: Nusu ya Waingereza hawajui kama Saudia imeanzisha vita dhidi ya Yemen
Mar 18, 2017 12:32Uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa unaonyesha kuwa zaidi ya nusu ya raia wa Uingereza hawana habari kuhusu vita angamizi vilivyoanzishwa na Saudi Arabia dhidi ya Yemen pamoja na kwamba serikali yao ni mmoja wa wauzaji wakuu za silaha zinazotumiwa na utawala wa Aal Saud katika vita hivyo.
-
Radiamali ya Iran kwa madai ya 'kipuuzi' ya Mwana Mfalme wa Saudia alipokutana na Trump
Mar 18, 2017 04:04Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekosoa vikali madai ya kipropaganda ya Riyadh na kuyataja kama ya kipuuzi na yasiyokuwa na msingi matamshi dhidi ya Tehran yaliyotolewa na Mwana Mfalme wa Saudi Arabia alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Marekani, Donald Trump katika Ikulu ya White House hivi karibuni.
-
UN, IOM zalaani mauaji ya wakimbizi 42 wa Kisomali, pwani ya Yemen
Mar 18, 2017 03:44Shirika la Kimataifa la Wahajiri (IOM) limekosoa vikali shambulio lililoua makumi ya wakimbizi raia wa Somalia katika pwani ya Yemen usiku wa kuamkia jana.