Ufaransa inaiuzia Saudia silaha za kuwaulia raia waliodhulumiwa wa Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i26678-ufaransa_inaiuzia_saudia_silaha_za_kuwaulia_raia_waliodhulumiwa_wa_yemen
Rais wa Ufaransa ametoa kibali cha kuuzia silaha utawala wa Aal Saud na hivyo kuuchochea waziwazi utawala huo kuendelea kuwauwa wananchi wa wasio na ulinzi na waliodhulumika wa Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 21, 2017 11:31 UTC
  • Ufaransa inaiuzia Saudia silaha za kuwaulia raia waliodhulumiwa wa Yemen

Rais wa Ufaransa ametoa kibali cha kuuzia silaha utawala wa Aal Saud na hivyo kuuchochea waziwazi utawala huo kuendelea kuwauwa wananchi wa wasio na ulinzi na waliodhulumika wa Yemen.

Rais Francois Hollande wa Ufaransa jana alitoa kibali cha kuiuzia silaha Saudi Arabia zenye thamani ya yuro milioni 455; ambapo sehemu kubwa ya silaha hizo zitatumika katika mashambulizi dhidi ya watu wa Yemen. Hii ni katika hali ambayo Baraza la Mawaziri la Ufaransa na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo zimepinga kutolewa kibali hicho cha kuiuzia Saudia kiwango hicho kikubwa cha silaha ambazo zitatumika kuishambulia Yemen. 

Itakumbukwa kuwa, mwaka 2016 Ufaransa ilikosolewa na baadhi ya nchi ilipotangaza kuwa imeagiza silaha za thamani ya Euro bilioni 20; na huku zikiashiria azimio nambari 2216 la Umoja wa Mataifa,  taasisi nyingi za kimataifa na zile zisizo za kiserikali zililaani vikali nafasi ya Saudi Arabia na nchi waitifaki wake katika kuendesha vita dhidi ya wananchi wa Yemen.

Watoto wa Yemen wanaotaabika kwa uvamizi wa kijeshi ulioanzishwa na Saudi Arabia nchini mwao 

Saudi Arabia ilianzisha uvamizi wa kijeshi huko Yemen tangu mwezi Machi mwaka juzi kwa kuungwa mkono na Marekani na nchi za Magharibi, na kuanza kuwauwa ovyo wanawake na watoto wa nchi hiyo maskini ya Kiarabu. 

Wakati huo huo Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) na taasisi za kutetea haki za binadamu zimeashiria kuuziwa Saudia silaha kutoka Uingereza, Marekani na Ufaransa kwa ajili ya kuendeleza mauaji dhidi ya wananchi wa Yemen na kulaani vikali hatua hiyo ya nchi hizo.