Aug 10, 2017 13:58
Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) amesema kuwa, kama Iran ikitaka kutoa jibu kwa ukiukaji wa makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Utekelezaji wa Pamoja (JCPOA) basi jibu lake litakuwa ni la kushtukiza.