Iran yazindua mafanikio 114 ya nyuklia
(last modified Tue, 09 Apr 2019 15:07:47 GMT )
Apr 09, 2019 15:07 UTC
  • Rais Rouhani (kulia) akiwa  na Mkuu wa Shirika la Atomiki la Iran Dkt. Ali Akbar Salehi wakati za uzinduzi wa mafanikio ya nyuklia nchini Iran, Aprili 09 2019, Tehran
    Rais Rouhani (kulia) akiwa na Mkuu wa Shirika la Atomiki la Iran Dkt. Ali Akbar Salehi wakati za uzinduzi wa mafanikio ya nyuklia nchini Iran, Aprili 09 2019, Tehran

Katika sherehe za 13 za Siku ya Kitaifa ya Nyuklia, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezindua mafanilkio 114 ya nyuklia nchini.

Ili kuenzi na kushukuru jitihada zilizojaa fahari za wasomi Wairani katika kuiwezesha nchi hii iweze kumiliki teknolojia ya nyuklia hasa kukamilisha mzunguko wa utegenezaji fueli ya nyuklia kwa malengo ya amani, tarehe 20 Farvardin  sawa na 9 Aprili huwa 'Siku ya Kitaifa ya Teknolojia ya Nyuklia.'

Kwa munasaba huo, Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran siku ya Jumanne alizundua mafanikio kadhaa ya nyuklia ikiwemo mashinepewa au centrifuge aina ya IR6, bidhaa inayojulikana kama Yttrium-90 ambayo ni muhimu sana katika matibabu ya saratani,oxygen-18 ambayo ni isotope imara inayotumika katika sekta ya madawa aina ya radiophamacueticals na spectograph ya FTIR (Fourier-transform infrared spectroscopy) ambayo hutumika katika sekta za tiba na chakula. 

Rais Rouhani (kushoto) akiwa  na Mkuu wa Shirika la Atomiki la Iran Dkt. Ali Akbar Salehi wakati za uzinduzi wa mafanikio ya nyuklia nchini Iran, Aprili 09 2019, Tehran

Mafanikio hayo na mengine ya nyuklia yamezinduliwa katika sherehe iliyohudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu serikalini na jeshini. Katika miaka ya hivi karibuni, sekta ya nyuklia ya Iran imeshuhudiwa mafanikio makubwa pamoja na kuwepo vikwazo vya kidhalimu dhidi ya nchi hii.

 

Tags