-
Jeshi la Sudan lasonga mbele katika jimbo la Nile ya Bluu baada ya mapigano na RSF
Sep 22, 2026 02:59Jeshi la Sudan limesonga mbele Jumatatu katika baadhi ya maeneo ya wilaya ya Kurmuk katika jimbo la kusini-mashariki la Nile ya Bluu kufuatia mapigano na waasi wa kundi la Askari wa Msaada wa Haraka (RSF) na mshirika wao, Harakati ya Watu ya Ukombozi wa Sudan-Kaskazini (SPLM-N).
-
IOM: Karibu Wasudan 100,000 wamekimbia makazi yao katika jimbo la Blue Nile
Sep 16, 2026 02:53Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limetangaza kuwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi sasa, karibu Wasudan 100,000 wamekimbia makazi yao katika jimbo la Blue Nile, kutokana na kuongezeka ghasia na mapigano katika eneo hilo.
-
Msaada wa kigeni kwa RSF ndio sababu kuu ya kuendelea kwa vita nchini Sudan
Sep 08, 2026 11:17Msaada wa nje kwa kundi la waasi la Rapid Support Forces (RSF) ndiyo sababu kuu ya kuendelea kwa vita vya muda mrefu na jinai nchini Sudan. Hayo yamedokezwa na mwanasheria mkuu wa nchi hiyo siku ya Jumatatu, akitoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua madhubuti za kukomesha hali hiyo.
-
WFP yalaani mashambulizi dhidi ya malori ya misaada kusini mwa Sudan
Sep 04, 2026 03:18Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) limetangaza kwamba malori yake mawili yalishambuliwa kutokea angani siku ya Jumapili nje ya eneo la Dilling la Jimbo la Kordofan Kusini, huko kusini mwa Sudan, wakati yalipokuwa njiani kupeleka chakula cha msaada kwa wakimbizi waliokwama kwenye eneo la Kadugli.
-
Shambulio la RSF dhidi ya msafara wa misaada wa UN Kordofan Kusini, Sudan lauwa mtu 1 na kujeruhi 2
Sep 03, 2026 10:15Wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) nchini Sudan wameshambulia msafara wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika jimbo la Kordofan Kusini, na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wengine wawili.
-
Karibu watu 20,000 wamelazimika kuhama makazi yao kufuatia kushtadi mapigano jimboni Blue Nile, Sudan
Aug 31, 2026 04:33Karibu watu 20,000 wamelazimika kuhama makazi yao katika jimbo la Blue Nile nchini Sudan kufuatia kuzorota hali ya usalama na kuongezeka hatari zinazowakabili wakazi wa eneo hilo. Haya yameripotiwa jana na shirika moja la misaada linalohudumu Sudan.
-
Sudan yafuta marufuku ya kutoka nje Khartoum, mafuriko yameharibu makumi ya nyumba Kordofan Kusini
Aug 29, 2026 02:46Serikali ya Sudan imetangaza kufutwa marufuku ya kutoka nje katika jimbo la Khartoum baada ya karibu miaka miwili ya utekelezaji wake kutokana na vita kati ya Jeshi la Taifa na waasi wa Rapid Support Forces (RSF).
-
Wapinzani Sudan wapinga mazungumzo ya kitaifa ya Burhan
Aug 26, 2026 03:30Mkutano mkubwa wa makundi ya kisiasa na asasi za kiraia za Sudan zinayopinga vita umemalizika huko Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia.
-
Malik Agar: Chaguo letu ni suluhisho la kijeshi hadi mazingira ya mazungumzo yatakapotimizwa
Aug 23, 2026 14:19Malik Agar, naibu mkuu wa Baraza Kuu la Utawala nchini Sudan, amesema kwamba chaguo la sasa ni suluhisho la kijeshi mpaka pale mazingira ya kufanyika mazungumzo yatakapotimizwa, akisisitiza kwamba Khartoum inalitaka kundi la Rapid Support Forces (RSF) kuondoka katika miji na maeneo ya makazi ya raia kabla ya mazungumzo yoyote kuanza.
-
Vita vya Sudan: Wapiganaji 318 wa RSF wajiunga na jeshi
Aug 20, 2026 03:21Jeshi la Sudan limeripoti kuwa wapiganaji 318 wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF), wakiwemo makamanda wanne wameasi na kujiunga na jeshi hilo katika tukio la hivi karibuni la wanachama wa kikosi hicho cha kijeshi kuamua kujisalimisha.