-
Katibu Mkuu wa UN alaani shambulio la anga Sudan lililoua watu 22 Omdurman
Jul 10, 2023 03:53Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani shambulizi la anga lililotokea Omdurman nchini Sudan, ambalo limeripotiwa kuua takriban watu 22.
-
Iran na Sudan kufufua uhusiano wao wa kidiplomasia karibuni
Jul 06, 2023 23:38Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekutana na kufanya mazungumzo na mwenzake wa Sudan kwa mara ya kwanza baada ya miaka saba, ambapo wamekubaliana kufufua uhusiano wa kidiplomasia wa nchio mbili hizi karibuni hivi.
-
Baraza la Usalama latakiwa kushughulia jinai dhidi ya raia katika mapigano ya Sudan
Jun 28, 2023 23:22Asasi na jumuiya 41 zenye mfungamano na wanawake Afrika, zimelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufuatilia na kushughulikia jinai dhidi ya raia nchini Sudan zinazofanywa na pande mbili hasimu katika vita vyao.
-
Kikosi cha RSF chasitisha vita Sudan kwa saa 48 kwa ajili ya Iddul Adh'ha
Jun 27, 2023 03:26Kikosi cha Radiamali ya Haraka cha Sudan (RSF) kimetangaza habari ya usitishaji vita wa upande mmoja wa saa 48 kuanzia leo Jumanne, kwa ajili ya maadhimisho ya Sikukuu ya Idul Adh'ha.
-
Pande hasimu Sudan zatakiwa kuweka silaha chini kuelekea Iddul Adh'ha
Jun 23, 2023 06:50Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imetoa mwito kwa vikosi hasimu vinavyopigana nchini Sudan kusitisha mapigano, wakati huu ambapo taifa hilo kama mataifa mengine ya Waislamu, linakaribia kuadhimisha Sikukuu ya Iddul Adh'ha (Iddul Hajj).
-
Wafadhili waahidi kutoa msaada wa dola bilioni 1.5 kwa ajili ya Sudan
Jun 20, 2023 04:35Wafadhili wameahidi katika Mkutano wa Geneva wa Kukabiliana na Mgogoro wa Sudan, kutoa msaada wa kibinadamu wa takriban dola bilioni 1.5, wakati huu ambapo hali ya utulivu imetanda kwa kiasi fulani nchini Sudan kwa siku ya pili kutokana na makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa baina ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).
-
Pande hasimu Sudan zafikia makubaliano mapya ya usitishaji vita ya saa 72
Jun 18, 2023 07:49Pande mbili zinazopigana nchini Sudan, jeshi la taifa SAF na kikosi cha uusaidizi wa haraka (RSF), zimekubaliana kusitisha mapigano kwa saa 72 kuanzia Jumapili ya leo.
-
Waliouawa katika mapigano ya Sudan wapindukia 3,000
Jun 18, 2023 04:03Wizara ya Afya ya Sudan imetangaza kuwa, idadi ya watu waliouawa katika mapigano yanayoendelea kushuhudiwa nchini humo ni zaidi ya elfu tatu.
-
UN: Zaidi ya 100 wameuawa katika mapigano Darfur Kaskazini, Sudan
Jun 16, 2023 04:12Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema watu zaidi ya 100 wameuawa kwenye mapigano katika jimbo la Darfur Kaskazini, magharibi mwa Sudan.
-
Sudan yakabiliwa na mgogoro mkubwa wa mahitaji muhimu huku vita vikiingia mwezi wa tatu
Jun 15, 2023 23:00Vita kati ya majenerali hasimu huko Sudan jana Alhamisi viliingia katika mwezi wake wa tatu na haijulikani lini vitamalizika. Ndege za kivita za jeshi la Sudan jana Alkhamisi zilifanya mashambulizi kwa mara ya kwanza katika mji wa kusini mwa nchi hiyo wa El- Obeid' na kuvituhumu Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kuwa ndivyo vilivyomteka nyara na kumuuwa Gavana wa Darfur.