-
OCHA: Mafuriko ya Sudan yameua watu 103, nusu milioni wameathiriwa
Sep 12, 2020 03:50Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imetangaza kuwa zaidi ya watu nusu milioni wa Sudan wameathiriwa na mafuriko makubwa yanayoikumba nchi hiyo kutokana na mvua kali zilizosababisha kujaa maji ya Mto Nile.
-
Sudan yaomba msaada wa kimataifa kwa waathiriwa wa mafuriko
Sep 08, 2020 11:52Waziri wa Afya wa Sudan ametahadharisha kuhusu uwezekano wa kujitokea maradhi ya kuambukiza katika siku kadhaa zijazo kutokana na maafa yaliyosababisha na mafuriko makubwa yanayoendelea nchini humo.
-
Malalamiko ya Sudan kuhusu mashinikizo ya Marekani ya kuwa na uhusiano na Israel
Sep 06, 2020 07:12Serikali ya Trump muda wote imekuwa ikijionesha ni mtumishi asiye na doa wa malengo ya utawala wa Israel na imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kama kuzilazimisha nchi za Kiarabu na za Waislamu kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala huo wa Kizayuni. Hata hivyo baadhi ya nchi kama Sudan zimeamua kupinga na pia kukabiliana na njama hizo.
-
Sudan na kundi kuu la waasi zakubaliana kuanzisha tena mazungumzo ya amani
Sep 04, 2020 22:03Serikali ya Sudan na kundi kuu la waasi linaloendesha harakati zake katika maeneo ya mpakani ya kusini mwa nchi hiyo zimeafikiana kuanzisha tena mazungumzo amani chini ya uwenyeji wa Sudan Kusini.
-
IGAD yafurahishwa na makubaliano ya amani ya Sudan
Sep 02, 2020 03:30Jumuiya ya Maendeleo ya Serikali ya Nchi za Afrika Mashariki IGAD imepongeza makubaliano yaliofikiwa hivi karibuni baina ya Serikali ya Sudan na Muungano wa Harakati ya Kimapinduzi kutoka jimbo la Darfur na katika majimbo ya kaskazini ili kuhitimisha mgogoro wa miaka 17 nchini humo.
-
Waasi wa Sudan waafiki makubaliano ya amani ili kuhitimisha mgogoro wa miaka 17 wa nchi hiyo
Aug 31, 2020 02:31Shirika la habari la Sudan limetangaza kuwa Muungano wa Harakati ya Kimapinduzi kutoka jimbo la Darfur na katika majimbo ya kaskazini umesaini makubaliano na serikali ili kuhitimisha mgogoro wa miaka 17 nchini humo.
-
Sudan yataka mzozo wa Bwawa la al-Nahdha ujadiliwe na marais wa nchi husika
Aug 30, 2020 07:29Serikali ya Khartoum imetoa mwito wa kujadiliwa mzozo wa Bwawa la al-Nahdha na marais wa Sudan, Misri na Ethiopia.
-
Safari ya Mike Pompeo nchini Sudan; juhudi za kuanzishwa uhusiano kati ya Khartoum na Tel-Aviv
Aug 27, 2020 03:10Licha ya juhudi za Mike Pompeo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani za kuifanya Sudan ikubali kuanzisha uhusiano rasmi wa kidiplomasia na utawala haramu wa Israel, lakini Abdalla Hamdok, Waziri Mkuu wa serikali ya muda ya Sudan amesisitiza kuwa, hana mamlaka ya kuchukua maamuzi kuhusiana na uhusiano na Israel.
-
Sudan yataka kuondolewa katika orodha ya ugaidi, yakataa kuanzisha uhusiano na Israel
Aug 26, 2020 01:38Serikali ya Sudan imetoa taarifa ikiiambia Marekani kwamba suala la kuondolewa jina la Sudan katika orodha ya magaidi halipasi kushurutishwa na kuanzisha uhusiano wa kidoplomasia na utawala haramu wa Israel.
-
Sudan iko tayari kushirikiana na ICC kuhusu jinai za kivita Darfur
Aug 23, 2020 03:26Serikali ya Sudan imesema iko tayari kushirikiana na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ili kuhakikisha kuwa washukiwa wa jinai za kivita katika eneo la Darfur wanafikishwa mbele ya korti hiyo yenye makao yake mjini Hague nchini Uholanzi.