-
Saudia: Sharti serikali ya Qatar itume vikosi Syria ili isipinduliwe
Apr 25, 2018 02:57Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia amesema iwapo serikali ya Qatar inataka isiondolewe madarakani na iendelee kudhaminiwa usalama na Marekani, sharti itume wanajeshi wake nchini Syria.
-
Shamkhani: Marekani na Ulaya zikivuka mstari mwekundu wa Iran zitagonga mwamba
Apr 24, 2018 22:02Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa nchini Iran amesema kuwa, iwapo Ulaya itafanya makosa ya kistratijia na kusalimu amri mbele ya Marekani na kuvuka mistari mnyekundu ya Iran kwa shabaha ya kutaka kumridhisha Donald Trump, hapana shaka kuwa itakula mweleka na kushindwa.
-
Trump aendelea kukosolewa, bunge la Ujerumani lalaani shambulizi la Marekani dhidi ya Syria
Apr 21, 2018 23:16Kinyume na serikali ya Ujerumani, bunge la nchi hiyo limelaani shambulizi la Marekani, Ufaransa na Uingereza dhidi ya Syria na kulitaja kuwa ni kukiuka sheria na mikataba ya kimataifa.
-
Jaberi Ansari afanya mazungumzo na mjumbe wa UN katika masuala ya Syria
Apr 21, 2018 09:38Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria leo amekutana na kufanya mazungumzo hapa mjini Tehran na Hossein Jaberi Ansar msaidizi mkuu wa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran katika masuala ya siasa.
-
Russia: Marekani na washirika wake wanafanya njama nyingi kuigawa Syria
Apr 20, 2018 23:06Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov amekosoa vikali misimamo ya uhasama ya Marekani ya kutaka ya kuisambaratisha nchi ya Syria.
-
Chokochoko za Marekani za kuzifungulia njia tawala za Kiarabu ya kujiingiza moja kwa moja kijeshi nchini Syria
Apr 20, 2018 03:22Bouthaina Shaaban, mshauri wa kisiasa na wa masuala ya habari wa Rais Bashar Al-Assad wa Syria ametoa jibu na radiamali kwa wito wa rais wa Marekani Donald Trump wa kutaka muungano wa vikosi vya nchi za Kiarabu ukashike hatamu za udhibiti wa eneo la kaskazini mwa Syria baada ya kuondoka wanajeshi wa Marekani.
-
Rais Assad arejesha nishani aliyopewa na 'Mtumwa wa Marekani'
Apr 20, 2018 02:54Rais Bashar al Assad wa Syria amerejesha nishani bora zaidi ya Ufaransa aliyotunukiwa na Rais Jacques Chirac mwaka 2001 na kusema hawezi kubakia na zawadi ya nchi ambayo ni mtumwa wa Marekani na ambayo imedondosha mabomu Syria.
-
Velayati: Baada ya muda si mrefu Yemen pia itajumuishwa kwenye kambi ya Muqawama
Apr 19, 2018 23:49Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema: kambi ya muqawama imepanuka kwa kuanzia Iran na kuenea hadi Palestina, Syria na Iraq; na muda si mrefu Yemen pia itajumuishwa kwenye kambi hiyo.
-
Russia: Makundi ya kigaidi Syria yanawazuia wakaguzi wa OPCW kuingia Douma
Apr 19, 2018 09:57Nabu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na nchi za kigeni huko Syria yanawazuia wakaguzi wa Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali (OPCW) kuingia katika mji wa Douma ulioko katika viunga ya mji mkuu wa nchi hiyo, Damascus.
-
CNN yafichua: Shambulio dhidi ya Syria lilifanywa bila kuwepo uhakika kama silaha za kemikali zilitumiwa Duma
Apr 18, 2018 22:33Ukiwa umepita muda wa chini ya wiki moja tangu Marekani na waitifaki wake waishambulie kijeshi Syria kwa madai ya kufanyika shambulio la silaha za kemikali nchini humo, kanali ya televisheni ya CNN ya nchini Marekani imefichua kuwa nyaraka na ushahidi uliotumiwa kwa ajili ya shambulio hilo ni picha tu na sampuli za vipimo visivyo vya moja kwa moja.