- 
        
            
            Sisitizo la Rais wa Tanzania kwa mkutano wa COP26: Tunapimwa kwa vitendo vyetu, si kwa ahadi kubwa kubwa tunazotoa
Nov 02, 2021 07:39Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaeleza viongozi wa mataifa ya dunia wanaohudhuria mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi COP26 huko Glasgow, Scotland, kwamba mshikamano na juhudi zao kama viongozi katika kukabili mabadiliko ya tabianchi vitapimwa si kwa ahadi kubwa wanazotoa kwenye mkutano huo bali kwa jinsi watakavyotekeleza vipengele vyote vya mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi.
 - 
        
            
            Rais wa Tanzania: Tutaendelea Kushirikiana na Burundi
Oct 22, 2021 14:43Tanzania imesema itaendelea kushirikiana na Burundi katika kuimarisha ulinzi katika mipaka ya nchi hizo mbili. Hayo yamesemwa na Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mazungumzo yake huko Chamwino Dodoma na Rais wa Burundi, Évariste Ndayishimiye ambaye yupo nchini humo kwa ziara ya siku tatu.
 - 
        
            
            Mamilioni ya Watanzania wanasumbuliwa na matatizo ya akili
Oct 10, 2021 07:56Tanzania inakadiriwa kuwa na watu milioni saba wenye matatizo yanayohusiana na afya ya akili. Hayo yamebainika wakati huu ambapo nchi hiyo ya Afrika Mashariki imejiunga na nchi zingine duniani hii leo kuadhimisha Siku ya Afya ya Akili.
 - 
        
            
            Rais Samia awaomba Watanzania ushirikiano katika kutekeleza ahadi zake UN
Sep 25, 2021 15:18Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameomba ushirikiano wa Watanzania ili kuyatekeleza kwa vitendo yale aliyoahidi katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York huko Marekani.
 - 
        
            
            Mahakama ya Tanzania yamfutia mashtaka ya uchochezi Tundu Lissu na wenzake watatu
Sep 22, 2021 13:37Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es salaam, Tanzania imefuta mashtaka dhidi ya makamu mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu na wenzake watatu, baada ya upande wa mashtaka wa serikali ya nchi hiyo kutangaza leo kuwa hauna nia tena ya kuendelea na mashtaka yote matano uliyokuwa umefungua dhidi ya washtakiwa hao.
 - 
        
            
            Rais wa Tanzania azindua kampeni ya uelimishaji kuhusu sensa ya mwaka 2022
Sep 14, 2021 12:26Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezitaka mamlaka zinazoshughulikia zoezi la sensa lililopangwa kufanyika mwakani kutumia gharama ndogo na kufanya zoezi hilo kwa ufanisi kwani serikali haina pesa ya kubeba gharama kubwa.
 - 
        
            
            Mkuu wa Jeshi la Polisi ya Tanzania: Polisi itakagua yanayofundishwa nyumba za ibada
Sep 11, 2021 13:30Jeshi la Polisi Tanzania limesema kuwa litakuwa likipita katika nyumba za ibada kukagua mafunzo wanayofundishwa watoto katika madrasa na shule za Jumapili (Sunday Schools) kufahamu aina ya mafundisho yanayotolewa.
 - 
        
            
            Baada ya miaka kadhaa, mara hii Rais wa Tanzania atashiriki mkutano wa Baraza Kuu la UN
Sep 04, 2021 08:00Kwa mara ya kwanza, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kushiriki katika mkutano wa kila mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambao katika ngazi ya viongozi wakuu, unatarajiwa kuanza tarehe 21 mpaka 27 za mwezi huu wa Septemba 2021.
 - 
        
            
            Polisi ya Tanzania: Hamza alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga, hakuwa na mgodi wala fedha
Sep 02, 2021 13:04Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema, Hamza Hassan Mohamed, aliyewaua askari polisi watatu na mlinzi mmoja wa kampuni ya SGA kisha kuuawa, alikuwa ni gaidi aliyejitoa kufia dini.
 - 
        
            
            Corona yapunguza muda wa vikao vya Bunge Tanzania
Aug 31, 2021 13:31Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepunguza muda wa kuanza kwa vikao vyake ambapo sasa litaanza vikao vyake kuanzia saa 8:00 mchana hadi saa 1:00 jioni, huku kukiwa hakuna kipindi cha maswali na majibu asubuhi ikiwa ni jitihada za kujikinga na ugonjwa wa Uviko-19.