Sep 11, 2021 13:30 UTC
  • Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro
    Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro

Jeshi la Polisi Tanzania limesema kuwa litakuwa likipita katika nyumba za ibada kukagua mafunzo wanayofundishwa watoto katika madrasa na shule za Jumapili (Sunday Schools) kufahamu aina ya mafundisho yanayotolewa.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro ameeleza hayo akizungumzia ziara yake ya siku nne katika nchi jirani ya Rwanda na kusema kuwa, wamejifunza hilo kutoka huko, hivyo ni vyema wapitie kwenye maeneo hayo kujua malengo ya mafunzo yanayotolewa.

Sirro amesema utaratibu huo 'ni mzuri' na kwamba watashirikisha viongozi wa dini na timu ya kupambana na makosa ya kigaidi kuona namna ya kupitia mafunzo yanayotolewa kwenye shule za dini na shule za elimu ya dunia hadi ngazi ya vyuo vikuu kuona kama mafunzo hayo yanawajenga au yanawabomoa vijana.

Vilevile ameitaka jamii kutoa taarifa endapo itabaini kuna mtu mwenye tabia au mwenendo kinyume na jamii husika, na kwamba sio lazima mhusika afungwe, bali anaweza kusaidiwa kuwa mtu mwema na akaendelea na shughuli zake.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro

Matamshi haya ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro yamezusha waziwasi wa kurejea katika zama za karne za kati wakati kanisa lilipokuwa likifanya taftishi na kukagua itikadi na imani za watu. Watu wengi hususan wasomi na wanafikra walipelekwa mahakamani na kudadisiwa imani na itikadi zao wakituhumiwa kuwa wameritadi na kuachana na Ukristo, kuwa washirikina au wachawi. Watu hawa kwanza walihukumiwa adhabu ya mateso makali na hatimaye walinyongwa na kuuawa kwa njia za kinyama na kikatili.  

Tags