Apr 30, 2024 11:10 UTC
  • Mwanasiasa mkongwe wa Uingereza: Sheria ya Rwanda inaharibu sifa ya Uingereza

Alfred Dubs mwanasiasa mkonge ambaye ni mjumbe katika Bunge la Malodi la Uingereza amesema kuwa mpango wa kuhamishia nchini Rwanda kutoka Uingereza raia wanaotafuta hifadhi si sahihi na hautafanikiwa.

Dubs amesema kuwa chama cha Labour kitabatilisha sheria hiyo iwapo kitashinda uchaguzi ujao nchini Uingereza. Naye James Wilson, Mkurugenzi wa kundi kwa jina la Detention Action ameitaja sheria hiyo mpya kwa wanaotafuta hifadhi kuwa ya kikatili na isiyo ya kibinadamu. 

Alfred Dubs ameitaja sera yenye utata ya serikali ya Uingereza kuhusu kuwahamishia nchini  Rwanda wanaotafuta hifadhi kuwa inakiuka haki za binadamu, utawala wa sheria nchini Uingereza na wajibu wa kimataifa wa nchi hiyo chini ya Mkataba wa Ulaya wa Haki za Kibinadamu. 

Mpango wa Uingereza wa kuwahamishia wakimbizi Rwanda 

Dubs ameeleza haya akiashiria  Sheria ya Usalama ya Rwanda, ambayo inaitaja nchi hiyo Kiafrika  kuwa mahali salama pa kupeleka wale wote wanaotafuta hifadhi.   

Dubs ambaye alizaliwa mwezi Desemba 1932 huko Pragueni kati ya watoto wa Kicheki waliokolewa kutoka kwa Wanazi huko Kindertransport katika mpango ambao uliwasaidia watoto wengine wa Kiyahudi wa Ulaya kutoroka na kukimbilia nchini Uingereza. 

 

Tags