May 18, 2024 07:39 UTC
  • Bagheri: Iran na Russia zimegeuza vikwazo vya Marekani kuwa fursa

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika Mkutano wa "Russia na Ulimwengu wa Kiislamu" kwamba: Vikwazo vya Marekani vimegeuzwa kuwa fursa kwa busara na viongozi wa Tehran na Moscow.

Mkutano wa " Russia na Ulimwengu wa Kiislamu" katika eneo la Kazan Tatarstan nchini Russia ulianza tangu tarehe 14 mwezi huu na unaendelea hadi kesho Jumapili. Lengo kuu la mkutano huo ni kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi, elimu na ufundi, uhusiano wa kijamii na kitamaduni kati ya Russia na nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na pia kuimarisha ustawi wa taasisi za Kiislamu za mifumo ya fedha ya Russia.  

Ali Bagheri Kani Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ambaye yuko safarini huko Russia amesema katika 'MKutano wa Russia na Ulimwengu wa Kiislamu' huko Kazan kuwa Russia na Iran zimefanikiwa kuvibadili vikwazo vya Marekani kuwa fursa si tu kwa ajili ya nchi mbili hizi pekee bali kwa ajili ya eneo zima. 

Ali Bagheri Kani, (katikati)

Bagheri ameongeza kuwa Marekani inazitishia nchi za eneo khususan Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia; ambapo inaendeleza vikwazo haramu dhidi ya nchi zote mbili ili kuziweka chini ya mashinikizo. Hata hivyo kwa busara ya viongozi wa Iran na Russia, vikwazo hivyo si tu vimekuwa fursa kwa nchi mbili hizi tu bali kwa nchi nyingine pia.  

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pia amesema: Haiwezekani kurejesha amani katika eneo bila ya kuzingatiwa masuala ya kiuchumi na kuwa Moscow na Tehran zitaedelea kuimarisha uhusiano wao. 

 

Tags